Alhamisi, 2 Juni 2016

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WAKUDHIBITI VITENDO VYAUKATILI.


Timothy Marko.
SERIKALI kwakushirikiana na asasi za kiraia mapema hii leo zimezindua muongozo wa kuratibu matukio yakesi za ukatili wakijinsia ikiwemo kupigwa kwawanawake naukatili wakingono unaofanywa na baadhi ya watuhumiwa wamakosa hayo yajinai yayolenga kudhalilisha utu wa mwanamke.

Akizungumza na waandishi wahabari mratibu wa mpango huo unaosimamiwa na taasisi isiyo yakiserikali taasisi inayojihusisha nausimamizi wa maendeleo ya Afya nchini (MDH)Emilian Busara amesema kuwa mpango huo wakudhibiti vitendo vya ukatili wakijinsia unalenga kuzikutanisha vyombo vya dola ikiwemo polisi ilikuweza kufanya uchunguzi wa matukio yaukatili wakijinsia.

''Muongozo huu wa Mdh unalenga kutoa andiko juu yaukatili wa kijisia ilikuweza kukomesha vitendo hivi kwakushirikiana najeshi lapolisi wizara yamambo yandani wizara yaafya ustawi wajamii pamoja wizara yajinsia na watoto ilkukomesha madhara yatokanayo naukatili wakijinsia .''alisema Emilian busara.
Takwimu zinaonesha kuwa Watatu kati ya wasichana 10 wamenyanyaswa kijinsia. -Asilimia 49 ya unyanyasaji wa kijinsia inafanyika katika makazi. -Asilimia 29 ya unyanyasaji wa kijinsia hufanyika wakati wa kusafiri kwenda/kutoka shule. -Asilimia 15.1 ya unyanyasaji hufanyika shuleni.

Mkoa wa Shinyanga umeendelea kutajwa kuwa ni moja ya mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni, vitendo vya ukatili wa kijinsia na mauaji kwa imani za kishirikina nchini hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kasi ya maendeleo kuwa ndogo miongoni kwa wakazi wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni