Jumatatu, 20 Juni 2016

MAUZO YA HISA JIJINI DAR ES SALAAM YAFIKIA BILIONI 4.9

Timothy Marko.


MAUZO ya  Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) imeongezeka kwa asilimia 76 kutoka sh.bilion 2.8 hadikufikia sh. bilioni  4.9 ambapo  Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa asilimia 20 hadi Milioni 2.2 kutoka Milioni 2.8.


Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja mauzo na Biashara, Patrick Mususa alisema kwa ujumla mauzo ya soko ya mekuwa ya kibadilika wiki hadi wiki kutokana na  wawekezaji wamekuwa kiji tathimini juu ya uwekezjiwao hasa kwa kuangalia mwenendo wa kampuni.


Amesema makampuni yaliyoongoza katika wiki ni  pamoja na Benki NMB kwa asilimia 47.85,  CRDB  asilimia 38.34 na kampuni ya Swissport  asilimia 10.00.


Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa soko umeongezeka asilimia 0.5 kutoka Trilioni 22.0 hadi Trilioni 22.1 ambapo ukubwa  mtaji wa makampuni ya ndani umepungua kwa asilimia 0.1 kutoka Trilioni 8.5 hadi kufikia  Trilioni 8.4


Aidha amesema Sekta ya viwanda (IA)  imepungua kwa pointi 2.72 ambapo  huduma za kibenki na kifedha (BI) zimeshuka kwa pointi 10.36 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za CRDB  kwa asilimia 1.33 wakati  huduma za kibiashara (CS) nazo zimeshuka kwa pointi 16.75 baada ya bei kushuka kwenye kaunta ya SWISSPORT 0.59.


Hata hivyoalisema mashindano ya Vyuo vikuu yanaendelea ambapo hadi sasa wanafuzi 3,160 kutoka vyuo mbali mbali wanaendelea na ununuzi na uuzaji wa hisa na bondi katika DSE Scholar Investment Challenge 2016


Mwanafunzi aliyekuwa anaongoza shindano hilo ameshindwa kutokana na mshiriki kutoka katika chuo cha SUA kuchukua nafasi hiyo na kuendelea kuwa wa kwaza katika wiki.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni