Jumatano, 9 Machi 2016

Jitokezeni kupima afya za watoto bila malipo.



Na Magreth Kinabo


Umoja wa Jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo nchini Tanzania wameandaa kambi ya upimaji wa afya bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa kushirikiana na kliniki  ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama,mtoto na vijana ya Mikocheni na Zahanati ya Kiugumo  itakayofanyika Machi 13 mwaka huu.


 Hayo yalisemwa leo na  Daktari Mstaafu wa Afya ya Jamii na Familia, Ali Mzige wakati akizungumza na waandishi wa  habari kuhusu  kambi hiyo ya kupima watoto bila malipo.


Dkt. Mzige alisema kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana jumla ya watoto 289 walipmwa afya zao wenye umri wa chini ya miaka mitano ambapo alisema asilimia tisa walipatwa maambukizi katika mfumo wa mkojo UTI. 


Aliongeza kwamba maambukizi hayo yanachangiwa na uvalishaji wan epi za watoto maarufu kwa jina la Pampers.


 Alisema asilimia saba walikatawa vimeo, asilimia tano walikutwa na utapia mlo.

 Dkt. Mzige alifafanua kwamba asilimia 20 ya watoto wenye umri katia ya miaka miwili hadi mine walikuwa na afya duni yya kinywa.


Aliishauri jamii  kuwa na tabia ya kufuata kanuni za afya na kuzingatia lishe bora ili kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni