Timothy Marko.
MAKAMU wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia SULUHU amesema kuwa serikali itaendelea na juhudizake zakumuwezesha mwanamke ikiwemo kupewa elimu kama nyenzo muhimu yakumkwamuwa mwanamke katika kupambana na maadui watatau ujinga maradhi na umasikini .
Kauli hiyo imetolewa mapema hii leo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke ambapo Makamu wa Rais SAMIA amesema serikali imepunguza kiwango cha ada mashuleni ili kuweza kuhakikisha wasichana wanapata fursa yakupata elimu .
''Serikali imepunguza mzigo wa ada mashuleni hii inamanisha wasichana wengi watapata fursa ya kupata elimu na kuhakikisha tatizo lausawa wakijinsia linasimamiwa ipasavyo katika ngazi zote za maamuzi ''Alisema Makamu wa Rais SAMIA SULUHU .
Alisema kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la wasischana Katika shule za msingi ,sekondari na vyuo idadi hiyo imekuwa niyakuridhisha wakati tanzania ikielekea katika dhana ya hamsini kwa hamsini kwa wanawake kwenye ngazi za maamuzi.
Makamu wa Rais SAMIA aliwataka wanawake kuwa nasauti moja katika kutokomeza vitendo vya ukatili wakijinsia ilivitendo hivyo vitokomezwe kabisa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni