Meneja MAUZO na Biashara Patrick Mususa |
SOKO la hisa
la Dar es salaam limewateua mabalozi wa vyuo vikuu kufuatia shindano la scholar
Investment challenge ili kuweza kutangaza huduma zinazotolewa na soko hilo .
Akizungumza
na waandishi wa Habari Mapema hii leo jijini Dar es salaam Meneja Mauzo na
Biashara amesema kuwa mabalozi walioteuliwa nipamoja na chuo cha IRP ,chuo
kikuu cha Dar es salaam ,sokoine ,IFM ,pamoja nachuo kikuu cha Dodoma
‘’Wanafunzi 500
wavyuo vikuu wameweza kushiriki katika shindano letu la Scholar Investment challenge
ambpo wanafunzi hawa watakuwa mabalozi wetu katika vyuo mbalimbali ‘’Alisema Meneja
Biashara na Mauzo Patrick Mususa
Mususa
alisema kuwa kupitia mabalozi hao wa vyuo vikuu nchini wataweza kukuza hamasa
kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali kuweza kushiriki katika shindano hilo .
Alisema kuwa
kila chuo kitakuwa namabalozi watano ambao watahamasisha wanafunzi kujiunga
nashindano hilo ambalo linaendelea .
‘’Ninatoa
wito wanafunzi wavyuo vikuu nchini kuweza kujitokeza katika shindano hili
ilikuweza kuwa mabalozi wetu wa soko lahisa ili kuweza kupata fursa mbalimbali
za kujijenga kiuchumi ‘’Aliongeza Mususa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni