Jumatatu, 8 Februari 2016

TAKWIMU :KIWANGO CHAMATUMIZI YA BIDHAA KATIKA NGAZI YA FAMILIA CHAPUNGUA .

Mkurungenzi wa ofisi ya Takwimu Ephraimu KWESIGABO

Timothy   Marko.

KIWANGO cha matumizi ya Bidhaa kwenye ngazi ya familia kimepungua kutoka asilimia 38.5 Kutoka asilimia 47.8 kwakipindi chamwaka 2011 ikilinganishwa 47.8 kwa mwaka 2007.


Akitoa takwimu hizo mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa ofisi ya Takwimu Epharaim Kusigabo amesema kuwa kutokana natakwimu hizo kiwango cha umasikini wakipato kimeweza kupungua katika ngazi ya familia nakuweza kuelekeza matumizi katika sekta za nishati na maji .

‘’Mizania ya matumizi ya familia kwenye bidhaa za vyakula imepungua lakini bado bidhaa za vyakula ndizo zinaongoza kwakuwa namizania kubwa ya matumizi kwa mwaka ‘’Alisema MKURUGENZI Epharaimu KUSIGABO.

Mkurugenzi KUSIGABO alisema kuwa makundi mengine yaliyoonesha matumizi makubwa kwangazi yafamilia nipamoja na usafiri 12.5 kutoka asilimia 9.5 kwamwaka 2007.makazi,maji ,pamoja na Nishati .

Alisema kumekuwa naongezeko lamatumizi kwangazi ya familia katika Nyanja yamawasiliano kwa asilimia 5.6 ikilinganishwa  na asilimia 2.1

‘’ Makundi mengine yaliyobaki hayakuwa na mabadiliko makubwa kutoka mwaka 2007 hadi 2011 wakati matumizi yakaya kilikuwa chini ya asilimia 7.0 ya familia kwa mwaka ‘’Aliongeza KWESIGABO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni