Ijumaa, 19 Februari 2016

NAPE ATUMBUA JIPU



Timothy Marko.  
Katika kuhakikisha utendaji unaimarika katika sekta ya michezo katika taifa Waziri wa Habari ,sanaa utamaduni na michezo Nape Nauye amemuondoa aliyekuwa mtendaji mkuu wa Baraza la michezo nchi(BMT) Henry Lihaya kwa kutowajibika ipasavyo katika usimamizi wa sera za michezo nchini.\

Akizungumza mapema hii leo jijini Dar es salaam Waziri Nape Nauye amesema kuwa uondoaji wa mtendajihuyo umefuatia kutowajibika katika kupitia sheria ambazo hazina manufaa kwa sekta yamichezo .

‘’Michezo ni sanaa tunafanya mabadilko katika baraza hili kwani baraza hili nimoyo wa sanaa ,kama hatutakuwa namipango hatuta weza endelea katika michezo ‘’Alisema Waziri wa Habari ,sanaa utamaduni ,michezo Nape Nauye .

Waziri Nape alisema kuwa ilikuweza kupiga hatua katika sekta hiyo nilazima kuwe na maaumuzi magumu ikuweza kusonga mbele nakufikia malengo yaliyo kusudiwa .

Alisema mara baada ya kutengua uteuzi wamtendaji huyo anatarajia atakaye teuliwa amabaye atashika nafasi hiyo atakuwa muwajibikaji nakuzifanyia marekebisho ya sheria zilizopitwa na wakati katika baraza hilo .
‘’Nitakaye mteuwa ninatarajia ataweza kubadilisha vifungu vya sheria ambazo zimepitwa nawakati nakuwa na katiba hizo ili tuweze kusonga mbele katika sekta yamichezo ‘’Alisema  Nape nauye .
KATIKA hatua nyingine Mwenyekiti wa Baraza lamichezo Dioniz Malinzi amemteua Saidi kiganja kuwa kaimu katibu mtendaji wa baraza hilo kufuatia waziri wa habari Utamaduni sanaa namichezo kutengua mtendaji mkuu Wa baraza lamichezo Herry  Lihaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni