Jumanne, 19 Januari 2016

WAANDISHI WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUHIFADHI MAZINGIRA.

Na Timothy Marko.

WAANDISHI wa Habari wametakiwa kutumia kalamu zao katika kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira ikiwa njia yakuondokana na magonjwa yamlipuko ikiwemo kipindu pindu .

Akizungumza katika mkutano wa andishi wa habari katika ukumbi wa idara maelezo jijini Mchugaji wa huduma ya Good News for all Leonard  Kajuna amesema kuwa waandishi ninguzo muhimu katika kuhamasisha wa kuu wa mipango miji na majiji kuweza kutumia taaluma zao katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na mipango miji .

‘’Waandishi wa Habari tumieni kalamu zenu katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira nakuweza kuhamasisha viwanda kuweza kupunguza hewa ya ukaa kwenye anga ‘’Alisema Mchungaji Leonard Kajuna .

Mchungaji Kajuna alisema kuwa kutokana na baadhi ya wananchi kuwepo kuweza kubomolewa nyumba zao kutokana kutozingatia sheria za mipangomiji hali inayopelekea baadhi ya wananchi hao kuweza kukaa katika mazingira yasiyo salama hali inayo pelekea kushindwa kwa baadhi ya miundombinu ya majitaka kushindwa na kusababisha magonjwa yamilipuko ikiwemo kipindupindu .

Alisema kupambana na tatizo la mipango miji nchini serikali haina budi kushirikiana na taasisi za kimataifa kuweza kuboresha makazi mazuri ilikuweza kuondokana na magonjwa yamlipuko ikiwemo kipindu pindu .


‘’SERIKALI inaratibu mipango miji lakini huruma inahitajika ikwemo kwa taasisi za kimataifa kutoamisada ya mahema kwa athirika wa bomoa bomoa katika maeneo yasiyo rasmi ilikuweza kupata makaazi bora ‘’Aliongeza Kajuna.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni