Ijumaa, 15 Januari 2016

SERIKALI YAWAHAMISHA WATUMISHI WA BANDARI ,KUBORESHA MAPATO.



Timothy Marko.
WAZIRI wa ujenzi ,mawasiliano nauchukuzi nchini Profesa Makame Mbarawa amewahamisha baadhi ya watendaji waliopo katika mamlaka ya bandari nchini (TPA)ilikuweza kuboresha ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia sekta ya Bandari .

Watumishi walio hamishwa katika mamlaka hiyo ya bandari nipamoja na Mkurugenzi wa Rasmali watu Peter Gawile kufuatia kuwepo nausimamizi hafifu waukusanyaji na usimamizi wa mapato yaserikali aidha watumishi wengine waliosimamishwa nipamoja na Mkurugenzi wa Tehama KALIANA CHALE pamoja na Mashaka kishana ambaye mkurugenzi wa manunuzi katika mamlaka hiyo .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salam Waziri Makame Mbarawa amesema kuwa sambamba nakuwahamisha watumishi hao wizara yake imeweza kuwateuwa Antony MBILINYI kuwaAFISA rasmali watu ,Benito Kalinga mkurugenzi wa manunuzi wakati huo huo ameweza kumteuwa Abdulahiman Bamba kama Mkurugenzi wa Tehama.

Waziri Mbarawa amesema kuwa serikali imeweza kusitisha huduma ya kampuni ya mawasiliano six telecom baada ya kutoza tozo kwa wateja wake tozo danganyifu kwa simu za nje .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni