Jumatano, 6 Januari 2016

OPERESHENI YA KUWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU KUANZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Timothy Marko .
JESHI lapolisi idara ya uhamiaji nchini imesema kuwa itaendesha  operesheni maalum ya kuwasaka wahamiaji haramu  jijini Dar es salaam ambao hawana vibali pamoja na wale wanaonfanya kazi ambazo zingetakiwa kufanywa na watanzania .
Operesheni hiyo inayotarajiwa kuanza mapema hii leo katika maeneo ya karikoo jijini Dar es salam inalenga kuwakamata wa hamiaji wote walioingia nchini pasipokuwa nakibali maalum  cha kuingia nchini .
Akizungumza jijini Dar es salam Naibu waziri wamambo ya ndani,  Hamad MASAUNI  amesema kuwa operesheni hiyo inafuatiwa baada ya wahamiaji haramu kujishughulisha na kazi za uzalishaji mali ambazo zingetakiwa kufanywa nawatanzania wenye utalaamu wa kufanya kazi zinazofanywa na wageni hao.
‘’IDARA ya uhamiaji itaendesha operesheni ya wahamiaji kuanzia leo katika maeneo ya Karikoo namaeneo yote ya jijini Dares salaam ,operesheni hii itajumuhisha wahamiaji ambao hawana vibali na wale walio kuwa na vibali vya muda mfupi vya kuishi hapa nchini na wale wageni wanaojihusisha nakazi ambazo zingetakiwa kufanywa na watanzania ‘’Alisema  Naibu WAZIRI Hamad  Masauni .
Naibu waziri Wa mambo yandani yanchi Hamadi MASAUNI amesema kuwa sambamba na operesheni hiyo pia ameitaka idara hiyo kuzingatia taratibu nasheria kwa wageni katika zoezi la utoaji wa vibali vya kazi .
Alisema kuwa sambamba nakutoa maagizo hayo pia aliiagiza iweze kutoa ripoti yautekelezwaji wamaagizo hayo nakuwataka idarahiyo kufanya kazi zake kisayansi zaidi.
‘’Lazima idara ya uhamiaji ifanye kazi zake kisayansi zaidi nakuna umuhimu wa maafisa uhamiaji kwenda eneo husika ilikuweza kubaini tatizo katika eneo husika ‘’Alisema Naibu waziri masauni .

WAZIRI Masauni amesema kuwa hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana idara ya uhamiaji inawashikilia jumla yawahamiaji182 ambao kati yao  waethopia 231  waliweza kukamatwa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni