Ijumaa, 10 Machi 2017

JAJI WARIOBA ATAKA NGUVU YA PAMOJA VITA YAMADAWA YAKULEVYA.

.

Tokeo la picha la warioba
jaji JOSEPH WARIOBA








Timothy Marko
MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba Jaji Mstaafu Joseph sinde Warioba amesema kuwa Vita ya  Madawa yakulevya nishirikishi kwajamii ya Kitanzania  nakuitaka serikali ya awamu yatano kuwekeza zaidi katika kutoa elimu katikangazi familia hadi kitaifa ilikuweza kukabiliana na janga hilo nchini.

Akizungumza katika hafla yauzinduzi wa kitabu cha Mtandao wa wanawake nakatiba Tanzania Jaji warioba amesema kuwa serikali inapaswa kuaelimisha jamii juu ya madhara yamadawa yakulevya kiwemo ulimaji wa madawa hayo ikiwemo bangi ambapo katika eneo la vijijini zao hilo limekuwa lakawaida kulimwa nawananchi kutojua madhara ya zao hilo.

''Kuna umuhimu wakuelimisha wananchi juu ya madhara yakulima bangi nilazima vita ya madawa yakulevya kuweza kujenga nguvu yapamoja kuweza kukomesha matumzi ya madawa yakulevya pamoja nausambazaji ''Alisema JAJI Joseph Warioba .

JajiWarioba amsema kuwa nilazima jamii lazima jamii ipewe elimu nanjia mbadala wa kuishi pasipo kutumia madawa yakulevya sambamba na juudi yakuyazuia madawa hayo yasiweze kupenya katika njia zapanya ndani na nje yamipaka ya nchi .

Alisema katika mapambano dhidi yamadawa yakulevya nivyema wanasiasa kuachana naitikadi zao nabadala yake kuweza kujenga nguvu yapamoja katika kuwabiliana najanga hilo .

Jumanne, 7 Machi 2017

VURUGU ZA MACHINGA ZAJERUHI WATU 9 JIJINI MWANZA WAKIWEMO MGAMBO WA JIJI.


 Na MWANDISHI WETU
Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa.

Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga.

Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.

Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri

JPM AWANYIMA USINGIZI ZANZIBAR


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK.JONH pombe  Magufuli

Wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likijipanga kuikatia umeme Zanzibar kama alivyoagiza Rais John Magufuli, SMZ inajipanga kuzungumza na shirika hilo ili kuona namna ya kulipa.

Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema yupo safarini na hakuzungumza kutokana na mawasiliano kuwa mabaya.

Baadaye mwandishi wetu alimtumia ujumbe mfupi, lakini Dk Mwinuka hakujibu.
Baada ya kukwama kupata maelezo ya Dk Mwinuka, mwandishi wetu alimtafuta kwa simu, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji ambaye alisema shirika hilo litatekeleza agizo la Rais kama alivyoagiza. “Rais ametoa kauli na kuagiza… lazima tutekeleze,” alisema Muhaji ambaye hakubainisha siku ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mohamed Aboud Mohamed alipoulizwa kuhusu deni hilo, alisema wamejiandaa kufanya mazungumzo kati ya mawaziri husika wa pande mbili za Muungano kuona namna wanavyoweza kufanikisha ulipaji wa deni hilo.

“Lengo letu ni kulipa deni lote kwa sababu ukidaiwa lazima ulipe. Tupo tayari kulipa ndiyo maana tumeanza kufanya mazungumzo na wenzetu wa Tanzania Bara, ili kuona namna tunavyoweza kukubaliana juu ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kulipa hatua kwa hatua ili kumaliza deni lote,” alisema.

Rais John Magufuli amemteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),



  1. UTEUZI: Rais John Magufuli amemteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Ikulu yaeleza.
  2. .

Ijumaa, 3 Machi 2017

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NA COMORO NCHINI,LEO IKULU JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt,ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais).  Picha ya pamoja  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Comoro hapa nchini Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais)

TRA YAINGIA MAKUBALIANO NA ZANZIBAR MAKUSANYO YA KODI.

Tokeo la picha la alphayo kidata
KAMISHINA WA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI( TRA)ALPHAYO KIDATA AKIZUNGUMZA NAWAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Timothy Marko
MA MLAKA  ya Mapato Nchini (TRA)imeaingia Makubaliano nachuo cha Kodi mjini Zanzibar ili kuweza kuwajengea watendaji waliopo mjini humo ili waweze kukusanya maduhuli ya serikali yatokanayo na kodi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamishina wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata amesema kuwa hatua ya kuwajengea uwezo watendaji wamamlaka hiyo waliopo katika chuo cha kodi mjini humo kitajumisha kozi 64 za mitaala yakodi iliyoidhinishwa na mamlaka hiyo .

''Mafunzo haya kwa watendaji wenzetu  wa kodi mjini Zanzibar yawawezesha kujijengea uwezo wama makusanyo yakodi ipasavyo nakuimarisha utendaji wao tuna tarajia kozi hizi za kuwajengea uwezo kuanza kikamilifu mwezi huu hadi mwezi juni mwaka huu''Alisema Kamishina wa TRA Aphayo KIDATA .

Kamishina wa Bodi ya Mapato Mjini Zanzibar Amir Bakari amesema kuwa Makubaliano hayo yanalenga kuwa jengea uwezo watumishi wa malaka hiyo kuweza kukusanya kodi ya mapato mjini humo.
Alisema hatua ya kuwajengea uwezo itajumuhisha  mafunzo mambali mbali ya Teknolojia ya ukusanyaji mapato nakusitiza kuwa tayari mandalizi yamafunzo hayo tayari yamekwisha kufanyika .
''Taasisi hizi mbili tayari zimeshaweka makubaliano ambapo matokeo ya makubalino hayo tanatarajiwa kuonekana hivi karibuni ''Alisema Amir .


Jumatano, 1 Machi 2017

BANDARI YA DAR ES SALAAM YAZINDUA MASHINE YAUKAGUZI WAMIZIGO .

Timothy Marko.
 Katika kuhahikisha sekta ya bandari inakuwa nakujenga uchumi katika nchi ya Tanzania JUMLA ya shilingi bilioni 20.28 zimetumika Kukarabati Mradi wa Scana uliopo katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na Tanga .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam Mhandisi Deus Kakoko wakati wauzinduzi wa mashine yaukaguzi mzigo bandarini hapo ambapo amesema kuwa uzinduzi wa Scana hiyo imetokana namsaada kutoka Jamuhuri ya watu wachina ili kuweza kukuza sekta ya bandari nchini .

''Scana hizi ambazo zimegharimu shilingi bilioni20.28 sambamba na Magari yaukaguzi wa bidhaa zinzoletwa bandarini umetokana na makubaliano yanchi mbili kati yachina na Tanzania ikiwa nijuhudi za nchi hizo kukuza sekta ya bandari sio Dar es salaam tu bali katika ukandakusini mwaafrika ambapo bidhaa nyingi hupita bandari ya Dar es salaam''Alisema Mkurugenzi Deusi Kakoko .

Mkurugenzi kakoko amesema upatikanaji wascana hizo katika bandari kutaweza kurahisisha zoezi lauhakiki kwa kipindi kifupi ambapo bidhaa moja itahakikiwa kwa saa moja nakupukana upotevu wamapato ya serikali yatokanayo nakodi .
Alisema Mradi huo utakuwa mwarobaini kwa wafanyabishara wanaohifadhi bidhaa zao katika bandari hiyo pasipo kulipa kodi stahiki yaushuru wa bidhaa bandarini hapo .
''Scana hizi zitasaidia ukwepaji wakodi nakuweza kutokomeza biashara haramu ya magendo ''Aliongeza KAKOKO.