Timothy
Marko .
JESHI
lapolisi idara ya uhamiaji nchini imesema kuwa itaendesha operesheni maalum ya kuwasaka wahamiaji
haramu jijini Dar es salaam ambao hawana
vibali pamoja na wale wanaonfanya kazi ambazo zingetakiwa kufanywa na
watanzania .
Operesheni
hiyo inayotarajiwa kuanza mapema hii leo katika maeneo ya karikoo jijini Dar es
salam inalenga kuwakamata wa hamiaji wote walioingia nchini pasipokuwa nakibali
maalum cha kuingia nchini .
Akizungumza
jijini Dar es salam Naibu waziri wamambo ya ndani, Hamad MASAUNI amesema kuwa operesheni hiyo inafuatiwa baada
ya wahamiaji haramu kujishughulisha na kazi za uzalishaji mali ambazo zingetakiwa
kufanywa nawatanzania wenye utalaamu wa kufanya kazi zinazofanywa na wageni hao.
‘’IDARA
ya uhamiaji itaendesha operesheni ya wahamiaji kuanzia leo katika maeneo ya
Karikoo namaeneo yote ya jijini Dares salaam ,operesheni hii itajumuhisha
wahamiaji ambao hawana vibali na wale walio kuwa na vibali vya muda mfupi vya
kuishi hapa nchini na wale wageni wanaojihusisha nakazi ambazo zingetakiwa
kufanywa na watanzania ‘’Alisema Naibu
WAZIRI Hamad Masauni .
Naibu
waziri Wa mambo yandani yanchi Hamadi MASAUNI amesema kuwa sambamba na
operesheni hiyo pia ameitaka idara hiyo kuzingatia taratibu nasheria kwa wageni
katika zoezi la utoaji wa vibali vya kazi .
Alisema
kuwa sambamba nakutoa maagizo hayo pia aliiagiza iweze kutoa ripoti
yautekelezwaji wamaagizo hayo nakuwataka idarahiyo kufanya kazi zake kisayansi
zaidi.
‘’Lazima
idara ya uhamiaji ifanye kazi zake kisayansi zaidi nakuna umuhimu wa maafisa
uhamiaji kwenda eneo husika ilikuweza kubaini tatizo katika eneo husika ‘’Alisema
Naibu waziri masauni .
WAZIRI
Masauni amesema kuwa hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana idara ya uhamiaji
inawashikilia jumla yawahamiaji182 ambao kati yao waethopia 231 waliweza kukamatwa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni