Ijumaa, 3 Machi 2017

TRA YAINGIA MAKUBALIANO NA ZANZIBAR MAKUSANYO YA KODI.

Tokeo la picha la alphayo kidata
KAMISHINA WA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI( TRA)ALPHAYO KIDATA AKIZUNGUMZA NAWAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Timothy Marko
MA MLAKA  ya Mapato Nchini (TRA)imeaingia Makubaliano nachuo cha Kodi mjini Zanzibar ili kuweza kuwajengea watendaji waliopo mjini humo ili waweze kukusanya maduhuli ya serikali yatokanayo na kodi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamishina wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata amesema kuwa hatua ya kuwajengea uwezo watendaji wamamlaka hiyo waliopo katika chuo cha kodi mjini humo kitajumisha kozi 64 za mitaala yakodi iliyoidhinishwa na mamlaka hiyo .

''Mafunzo haya kwa watendaji wenzetu  wa kodi mjini Zanzibar yawawezesha kujijengea uwezo wama makusanyo yakodi ipasavyo nakuimarisha utendaji wao tuna tarajia kozi hizi za kuwajengea uwezo kuanza kikamilifu mwezi huu hadi mwezi juni mwaka huu''Alisema Kamishina wa TRA Aphayo KIDATA .

Kamishina wa Bodi ya Mapato Mjini Zanzibar Amir Bakari amesema kuwa Makubaliano hayo yanalenga kuwa jengea uwezo watumishi wa malaka hiyo kuweza kukusanya kodi ya mapato mjini humo.
Alisema hatua ya kuwajengea uwezo itajumuhisha  mafunzo mambali mbali ya Teknolojia ya ukusanyaji mapato nakusitiza kuwa tayari mandalizi yamafunzo hayo tayari yamekwisha kufanyika .
''Taasisi hizi mbili tayari zimeshaweka makubaliano ambapo matokeo ya makubalino hayo tanatarajiwa kuonekana hivi karibuni ''Alisema Amir .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni