Jumatano, 16 Desemba 2015

SERIKALI YAWATAKA WATENDAJI WAMIJI KUTEKELEZA AGIZO LA KUTEKETEZA TAKA ZILIZO KUSANYWA DESEMBA 9

Timothy Marko. SERIKALI imezitaka halimashauri za miji kuweza kutekeleza agizo la uteketezaji wa taka zilizo kusanywa katika maeneo mbalimbali katika kutekeleza agizo la Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania JONH POMBE MAGUFULI alilolitoa katika maadhimisho ya siku ya uhuru Desemba9 mwaka huu kuwa ni siku ya usafi . Akitoa agizo hilo mapema hii leo jijini Naibu waziri wa afya naustawi wajamii KHAMIS KiGWANGALA amesema kuwa halimashauri zote zamikoa zinatakiwa kutekeleza agizo hilo la uteketezaji wa taka hizo ndani yakipindi cha wiki moja . ‘’Ninawaagiza watendaji wa halimashauri za miji kutekeleza katika agizo nililotoa leo la kuhakikisha kuwa kila halimashau ri inasimamia kutekeza taka zote nakuzikusanya sehemu maalumu badala ya kuzikusanya taka hizo ‘’Alisema KHAMIS KIGWANGALA . Naibu waziri Wa afya Kigwangala alisema kuwa hali yakipindupindu nchini imekuwa siyakuridhisha na kuwataka watendaji hao wa Halimashauri kuzingatia kanununi za kuimarisha nakudumisha hali ya usafi kama walivyoweza kutekeleza agizo laRais alivyolitoa desemba 9 mwaka huu . KATIKA hatua nyingine waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kuwa hadi kufikia jana takwimu zinaonesha kuwa kumekuwepo wagonjwa wapya wakipindupindu 141nakuweza kusabababisha vifo viwili na mikoa inayo ongoza nipamoja na Mara mbeya kigoma pamoja na Mwanza .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni