Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 28 Desemba 2015
SERIKALI :HATUJA SITITISHA HUDUMA ZA DK MWAKA ,TUNAHITAJI ASAJILI DAWA ZAKE
Timothy Marko.
SAKATA la utoaji wa Dawa za asili za mitishamba la Dr.Mwaka limechukua sura mpya baada ya serikali kukiri wazi kuwa halijasitisha huduma za Dakitari huyo wa tiba za mitishamba nabadalayake kuwataka wamiliki na watoaji huduma za tiba asili kuthibitisha dawa zao katika wizara ya afya ili ziweze kutumika kwa manufaa ya binadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Waziri wa afya na ustawi wa jamii Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali inaitambua huduma yatiba asili kama ilivyo anishwa nasheria 23 (2002)yatiba za asili nakuanishwa wazi juu ya utendaji kazi wa taasisi hizo .
‘’Tunazo sheria ikiwemo sheria ya mwaka 2002 kifungu cha 23 cha tiba asili kinaeleza wazi juu yautendaji wa taasisi zote zinazojihusisha na tiba mbadala ‘’Alisema Waziri Ummy Mwalimu .
WAZIRI Mwalimu alisema kuwa sheria za mtoaji wa tiba asili zinamtaka mtoaji wa huduma hiyo kusajili dawa kabla yakutoa dawa hizo kwa wananchi .
Alisema kutokana na sheria hiyo hakuna mganga wa tiba asili atakaye ruhusiwa kutoa huduma ikiwemo dawa kama dawazake hazija sajiliwa na mamlaka ya dawa Tfda ama wizara ya afya.
‘’Kama kuna wadau wamekwazwa na agizo hili nililo litoa ninaomba tukutane kwenye meza ya majadiliano ili tuweze kujadili suala hili ‘’ Aliongeza WAZIRI wa afya Ummy MWALIMU .
MWalimu Aliongeza kuwa serikali haiwezi kupiga marufuku tiba hiyo ya asili nakusitiza kuwa serikali pamoja na waganga watiba asili ni wadau muhimu katika sekta ya afya
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni