Jumanne, 24 Novemba 2015

TACAIDS:MAKUNDI HATARISHI NIKIKWAZO CHA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Timothy Marko. KUFUTIA Maadhimisho yasiku ya ukimwi yanayotarajiwa kufikia kilelechake Desemba mosi M waka huu Tume ya Taifa yakudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS )imesema kuwa kundi lavijana wenye umri kati ya miaka 19 hadi 24 lipo katika hatari kubwa yakuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU). Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti ukimwi Fatuma Mrisho amesema kuwakundi kubwa linalo kabiliwa na changamoto ya maambukizi ya ukimwi nipamoja nakundi la vijana wanajihusisha na madawa ya kulevya ,wasichana wanaofanya biashara yangono ,wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile . ‘’Wakati tukielekea katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani Desemba mosi mwaka huu bado tuna kabili liwa changamoto yakundi hatarishi ikwemo wasichana awanofanya biashara ya ngono asilimia 26,ngono jinsia moja 22,wakati wanaujidunga sindano ni asilimia ni asilimia 15’’Alisema Mkurungenzi wa TAC AIDS Fatuma Mrisho . Mkurugenzi Fatuma Mrisho alisema kuwa kundi kubwa ambalo lipo katika hatari kubwa nipamoja na wanawake wanaofanya biashara yangono ,nakusisitiza kuwa taasisi hiyo imelenga kutoa elimu elekezi juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi . Alisema kuwa ilikuweza kufikia maambukizi 000 nilazima jitihada za dhati ziweze kutumika ikiwemo waandishi wa habari kuweza kuripoti habari sahihi juu ya mwenendo wa juhudi za serikali ikiwemo taasisi hiyo katika kudhiti suala la mambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kundi hilo hatarishi . ‘’ Waandishi wahabari ninawaomba mtumie wiki ya maadhimisho ya siku ya ukimwi yanayotarajiwa kufanyika Desemba mosi mwaka huu katika kuandika makala mbalimali kusiana na jitihada za serikali katika kupambana virusi vya ukimwi ‘’ Aliongeza Mkurugenzi Fatuma Mrisho .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni