Ijumaa, 14 Agosti 2015

JESHI LA WANANCHI WATANZANIA (JWTZ)LAKANUSHA KUJIHUSISHA NA MASWALA YAKISIASA.

Timoth Marko.
KUFUATIA kauli iliyotolewa na katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Jonh Mnyika kuwa jeshi la wananchi watanzania (JWTZ)limewanyang'anya kadi za kupigia kura baadhi ya maofisa wake,jeshi hilo limekanusha madai ya mbunge huyo .
Akizungumza nawaandishi wa Habarimapema hii leo jijini Dar es Salaam,mkurugenzi wa mawasiliano wa jeshi hilo Cop ,Nelson Lubinga amesema kuwa jeshi lake hali yawahi kufanya vitendo vya namna hiyo nawala halitotarajia kufanya hivyo.
''Jeshi linalomajukumu yalioko wazi,kwamujibu wataratibu wa jeshi la JWTZ Jeshiletu linaheshimu haki za kikatiba nakumuheshimu mwanajeshi kama raia wa kawaida wa Tanzania,Hivyo anayo haki yakumchagua kiongozi anaye mtaka ''Alisema Nelson Lubinga
Lubinga alisema kuwa kwamujibu washeria wanajeshi hawarusiwi kuwa na itikadi ya chama chochote cha siasa nakusisitiza jeshi hilo linafuata taaratibu za kijeshi ambazo zinajulikana dunia nzima .
alisema kufuatia kauli hiyo jeshi hilo limesikitishwa na kitendo cha mbuge huyo Jonh Mnyika ambaye nimbunge wa chama cha upinzani nchini Tanzania .
''Tunaomba wanasiasa mfanye kazi zenu za kisiasa hoja zenu zijikite katika maeneo ya kisiasa kwani lugha hizo zina leta ukakasi ,hofu na wasiwasi kwa wananchi ''Aliongeza Lubinga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni