Ijumaa, 13 Februari 2015

CUF YASITISHA MAANDAMANO


Timothy Marko .
JESHI lapolisi kanda maalum mkoa wa Dar es salaam limeweza kudhibiti maandamano yaliyopangwa kufanyikia mapema hii leo na jumuhia yavijana  wa chama cha wananchi (JUVICUF) baada yakufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa chama hicho nchini Professa IBRAHIM Lipumba na jeshi hilo .

Akizungumza juu yausitishwaji wa maandamano hayo mapema hii leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es salaam  kamishina wa polisi wakanda maalumu Suleiman Kova amesema kuwa baada ya mwenyekiti huyo wa chama cha wananchi kupata taarifa kutoka kwajeshi hilo aliwataka uongozi wa JUVICUF kusitisha maandamano ilikuweza kuepusha matatizo yasiyo yalazima .
‘’Mwenyekiti wa wa CUF taifa professa Ibrahim lipumba amenijulisha mimi kuwa ameshazungumza nauongozi wa  JUVICUF ili waachane na maandamano ilkuepusha matatizo yatakayoweza kutokea ‘’Alisema Suileima  KOVA.
Kamanda  KOVA alisema kutokana namawasiliano baina yake na kiongozi wa chama hicho nakubaini kuwa endapo maandamano hayo yangefanyika yangeweza kuleta madhara makubwa .
Alisema kuwa anawashukuru wanachama wachama hicho pamoja nakiongozi wachama hichokutumia busara yakutofanya maandamano kwani mapambano kati yaw a nachama hao kungeweza kufanya uvunjifu wa amani .
‘’Mimi naamini kwamba huu ni ukurasa mpya uliofunguka nakutoa fursa baina yapande mbili jeshi lapolisi na chama cha wananchi CUF ‘’Aliongeza kamanda kova.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni