Timothy
Marko
Mwenyekiti wa chama cha wananchi nchini CUF
Profesa Ibrahimu Lipumba amemtaka Rais Jakaya kikwete kuwaangalia watendaji
wake waliopo chini yake juu ya utendaji wao katika usimamizi wa chaguzi
mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu ujao kufuatia kasoro zilizojitokeza katika
uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni .
Akizungumza mapema hii leo jijini Dar es salaam Professa
Ibrahimu Lipumba amesema kuwa kumekuwa matukio yambinu chafu katika uchaguzi
katika serikali za mitaa ikwemo ucheleweshwaji wa vifaa vya uchaguzi nakufanya
uchaguzi huo katika serikali za mitaa kuahirishwa kutokana kutofika vifaa vya
uchaguzi ikiwemo karatasi za kupigia kura kuchelewa kufika katika vituo vya
kupigia kura .
‘’wilaya nyingi chaguzi hazikuanza kwa wakati
kutokana nauchelewesh waji wavifaa katika vituo mbalimbali nakuweza kuathiri
uchaguzi ikiwemo uchaguzi kusogezwa mbele ‘’Alisema Profesa Ibrahim Lipumba
.
Professa Lipumba alisema kuwa katika mikoa
mbalimbali ikwemo Dar es salaam katika kata yailalavingunguti ,Na baadhi ya
kata mbali mbali katika mikoa kulionekana kasoro za wazi kama kata za kishapu ,mkinga
,tunduru ulanga ,kasulu ,zilionekana kuwa na kasoro uchaguzi .
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni