Ijumaa, 19 Septemba 2014

JUKWAA LA WAHARIRI LA LAANI VIKALI TUKIO LAKUPIGWA WAANDISHI WA HABARI KWENYE MAHOJIANO KATI MWENYIKITI WA CHEDEMA NA JESHI LA POLISI


Timothy  Marko.
KUFUATIA jeshi la polisi nchini Kudaiwa kuwapiga waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao katika kufuatilia mahojiano maalum na MWENYIKITI  wa chama cha Demkrasia na maendeleo(CHADEMA) FREEMAN MBOWE,  JUKWAA la wahariri nchini limeitaka jeshi hilo kujinasua katika tuhuma nzito kwa kuwaondosha maafisa wake wanaotuhumiwa kuwapiga waandishi.
Akizungumza na waandshi wa habari mapema hii leo, Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini TEF Absalom kibanda amesemakuwa kutokana najeshi hilo kuwa kimya imeonesha wazi walihusika natukio hilo la kuwa shambulia waandishi wa habari katika tukio lililofanyika jana .
‘’Jeshi lapolisi linapaswa kufanya kile kilicho fanywa napolisi wenzao wa Brazill julai mwaka huu ambako askari polisi wanne  walionaswa katika mikanda ya video wakiwashambulia waandishi wa habari walisimamishwa kazi ilikupisha uchunguzi dhidi yao ‘’Alisema Absalom kibanda
Kibanda alisemakuwa wataendelea kutumia kalamu zao na zananyingine za kikazi kulaani matukio hayo aliliyofanywa najeshi hilo kwakuwashambulia waandishi wa habari pamoja na athari zake kwa umma ili umma utoe hukumu inayostahili kwa jeshi hilo.
Alisema kuwa serikali inapaswa kuchunguza kwakina matukio hayo ya jeshi lapolis kuwa shambulia waandishi wa habari ilikujua hasira za polisi dhidi ya waandishi zina tokana na nini wanataka kuficha nini watathimini athari zake katika mfumo mzima wautoaji na upatikanaji wa habari nchini .
‘’jukwaa linaamini kuwa yeyote mwenyesilika za ukiukwaji wa haki za binadamu zikiwemo za namna hii za kuwashambulia waandishi anakwenda kinyume cha wajibu wake nayeye mwenyewe anavimelea vya uhalifu’’Aliongeza Kibanda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni