Timothy Marko.
Zaidi ya
shilingi bilioni 77.5 zitatumika katika kuboresha miundombinu ya reli ya
TAZARA ambapo fedha hizo zimetokana na
makubaliano ya nchi mbili kati ya japan na nchi ya Tanzania katika kuboresha
miundo mbinu hiyo ikiwa ni mkakati wa kufikia katika mpango wa maendeleo wa
matokeo makubwa sasa.
Akizungumza
nawaandishi wahabari jijini Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa wizara yafedha
Servanus Likwelile amesema kuwa sambamba na fedha hizo pia serikali ipo katika
kuboresha sekta yamiundo mbinu ikiwemo barabara za juu pamoja na kuboresha
miuundombinu katika sekta ya umeme katika jiji la Dar es salaam.
‘’Serikali
ya japan imetoa msaada wa jumla shilingi bilioni 77.5 kwa ajili yakudsaidia
miradi mbalimbali Ikiwemo mradi wa kuboresha miundo mbinu ya reli ya Tazara pamoja
na mradi wa bara bara za juu maarufu kama ‘’Flyover’’sambamba na mradi wa
kuboresha sekta ya umeme jijini Dar es salaam’’Alisema Servanus Likwalile .
Katibu Mkuu
wizara ya fedha Servanus Likwalile alisema kuwa
fedha hizo pia zitatumika
kutengeneza bara bara za juu ambapo zaidi milioni 52 .55 Bilioni zinatajiwa
kutolewa ilkuweza kufanikisha mradi huo wa barabara za juu maarufu kama
Flyover.
Alisema
jumla ya shilingi bilioni71.9 zinatajiwa kutolewa kutoka serikali ya japani
ilikuweza kuboresha miradi mbalimbali ikiwem omiradi ya umeme katika mkoa wa
Dar es salaam ambapo jumla ya vituo
viwili vya kusambaza umeme vinatajiwa kujengwa katika maeneo ya Muhimbili
,Mwananyamala na jangwani beach ambapo nisawa nakilometa za mraba 17.2 zenye
uwezo wakubeba 33kv kwavituo vitatu.
‘’Kuimarika
kwa miradi hii kutawezsha kuondokana na changamoto ya ukatikaji wa ummeme jijini
Dar es salaam na kuimarisha ukuwaji wauchumi katika mkoa huu ‘’Aliongeza katibu
wa wizara yafedha,
KATIKA hatua
nyingine ,jumuhia ya ulaya nchini imeipatia serikali ya Tanzania magari 21
ambayo yanajumla ya thamani bilioni 1.4 kwajili kuboresha sekta yakilimo kwa
wakulima akiwakilisha msada huo Muwakilishi wa jumuhia hiyo ya ulaya nchini
Tom venus amesema kuwa msaada huo unalenga kuboresha sekta ya miundo
mbinu katika kuboresha sekta ya kilimo nchini ikiwemo kusafirisha mazao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni