SAFARI ZA UTALII , SERENGETI NA RUAHA IRINGA ZAONGOZA
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe (
kulia) akimakabidhi Bi Jane Mwakinyuke kutoka Hifadhi ya Taifa Mikumi ,
cheti cha kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja ya kuongoza watalii
katika hifadhi za Taifa
Askari pekee wa kike kutoka hifadhi ya Taifa ya Ruaha Jane Griffin Mwakinyuke ambae amehitimu mafunzo ya kuongoza watalii katika utalii wa miguu hifadhini akionyesha cheti chake |
……………………………………………….…Na FRANCIS GODWIN BLOG……………………………………………………………………..
TANZANIA yazidi kung’ara
katika sekta ya utalii barani Afrika baada ya kuwa nchi ya kwanza
barani Afrika kwa kwa kuvutia zaidi watalii katika safari za
utalii katika hifadhi hiyo huku hifadhi ya Serengeti na Ruaha Iringa
zikiongoza kwa ubora ya utalii.
Dr
Dembe alisema kuwa Tanzania imeonekana ni nchi ya kwanza kwa utalii
baada ya wataalum wa masuala ya utalii barani Afrika kuchagua
nchi nane barani Afrika ambazo zinafaa kwa kufanya safari za utalii
Alizitaja
nchi zilizoshindanishwa kwa kupigiwa kura kuwa ni Tanzania ,
Botswana , Uganda , Namibia ,Afrika ya kusini , Kenya , Zambia na
Zimbabwe na huku Tanzania ikionekana ni nchi inayoongoza kwa
safari za kitalii ukilinganisha na nchi nyingine zilizowekwa katika
orodha hiyo.
Pia
alisema mbali ya kuchagua nchi inayofaa kwa utalii pia wataalam hao
walitazama maeneo 50 yaliyofaa kwa safari za utalii na Tanzania
ikifanikiwa kupata maeneo 10 bora zikiwemo hifadhi 8 ambazo zipo
katika TANAPA na Selous na Ngorongoro huku mlima wa
Kilimanjaro haukuwekwa kutokana na hifadhi hiyo ya Kilimanjaro ni
maalum kwa kupanda mlima pekee.
Hata
hivyo alisema katika hifadhi hizo 10 bora kwa hifadhi za kusini
hifadhi ya Ruaha imeongoza ikifuatiwa na katavi wakati hifadhi ya
kwanza kwa hifadhi bora ilikuwa ni Serengeti wakati hifadhi ya
pili ilikuwa ni hifadhi ya Ruaha barani Afrika ambazo zilionekana ni
bora na vinavutia zaidi kwa safari za kitalii.
Dr
Dembe alisema kuwa hivi sasa TANAPA wameelekeza nguvu zote
katika kuendelea kuitangaza hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni
pamoja na kubadilisha mazingira ya hifadhi hiyo ili kuvutia idadi
kubwa ya watalii katika hifadhi hiyo ambayo ndio hifadhi kubwa
kuliko zote katika Tanzania.
Hata
hivyo alisema kuwa katika kuboresha utalii wa kusini TANAPA ipo
katika mkakati wa kutoa elimu kwa madereva wanaopeleka wageni
katika hifadhi mbali mbali ikiwemo hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ili
kuona kampuni za kitalii kuwa na madereva ambao wanajua vema utalii
na kuepuka udereva wa vurugu katika hifadhi.
Alisema
kuwa utalii ni sekta nyeti katika Taifa hivyo lazima wale wote
wanaohusika na masuala ya utalii kuwa na elimu ya kutosha juu ya
utalii na kuyataka makampuni kuepuka kuwatumia madereva wa daladala
kupeleka wageni hifadhini ambao baadhi yao wamekuwa hawana elimu ya
utalii .
Kuhusu
askari hao 20 waliopewa mafunzo Dr Dembe aliwataka kuwa
wazelendo na hifadhi pamoja na Taifa zima la Tanzania na kuepuka
kugeuka kuwa maadui wa hifadhi kwa kushirikiana na majangili
kuhujumu hifadhi hizo .
Wakati
huo huo Dr Gembe alivitaka vyombo vya habari na wanahabari nchini
kuendelea kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na kuepuka kuandika
habari ambazo hazisaidii katika ukuzaji wa sekta ya utalii .
Alisema
iwapo vyombo vya habari nchini vitafanya vizuri katika
kuhamasisha utalii na kuwa na uzalendo na Taifa la Tanzania katika
kuepuka kuandika habari za kutisha wageni kufika katika hifadhi ni
wazi sekta ya utalii nchini haitakuwa .
Kaimu
mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ruaha Bw John Nyamhanga mbali ya
kuomba TANAPA kusaidia kumaliza kero ya vitendea kazi kwa askari hao
bado alisema kuwa mafunzo hayo ya utalii wa miguu kwa askari hao
ni mzuri zaidi japo mafunzo hayo yanaweza kukwamisha upande mmoja
katika utendaji kazi wa kila siku katika hifadhi hiyo ya Ruaha .
Kwani
alisema kuwa askari hao ndio ambao wamekuwa wakitumika katika
shughuli nyingine za hifadhi hiyo hivyo iwapo TANAPA haita ongeza
idadi ya watumishi wengine kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya
watumishi wa idara nyingine .
Godwell ole Meing’ataki Mratibu wa
mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa
Tanzania. ‘ SPANEST alisema kuwa lengo la SPANEST ni kuendelea
kuboresha zaidi hifadhi ya Ruaha ni nyingine ili kuwavutia zaidi
watalii wa ndani na nje kufika katika hifadhi hizo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni