NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAIS Ngosi Mwihava. |
Timothy
Marko.
NAIBU Katibu
Mkuu ofisi ya Rais nchini Ngosi Mwihava amewataka vijana kujikita katika
utunzaji wa Mazingira ilikuweza kuondokana natatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi
.
Mwihava
aliutoa wito huo wakati akizungumza nawaandishi wa habari jijini Dar es salaam
juu yaumuhimu ya utunzaji wa mazingira na kuweka katika uoto wa asili ambapo
alisema kuwa shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zina changiwa na
shughuli mbalimbali zakibinadamu ambapo mara nyingi zimekuwa zikichangia
uharibifu wa mazingira .
‘’Masuala ya
mabadiliko ya tabia yanchi yanachangiwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo
uchomaji wa misitu kwa ajili yamkaa ,hivyo natoa wito kwa vijana kufanya kazi
katika kujenga uchumi huku tukizingatia utunzaji wa mazingira kwa vizazi
vijavyo ‘’Alisema Naibu Katibu Mkuu Ngosi Mwihava
Naibu Katibu
Mkuu Mwihava alisema kuwa zaidi ya hekta tatu hadi saba za misitu hupotea
kutokana nashughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa misitu kwa ajili shughuli
za kibinadamu ikiwemo kilimo nabiashara ya mkaa hali inayopelekea uharibifu wa
kimazingira .
Alisema kuwa
katika kupambana na tatizo hilo ,serikali imejipanga kupambana na uharibifu wa
mazingira ikiwemo kuhamasisha upandaji wa miti na uhifadhi wa misitu
.
‘’Katika
kufanikisha suala hili la utunzaji wa mazingira serikali imeweza kupigamarufuku
suala zima la matumizi yamifuko ya plastiki kwa kutumia vyombo vya sheria
ikiwemo polisi ilikuweza kusimamia sheria mbalimbali za utunzaji wa mazingira ‘’Aliongeza
Ngosi Mwihava .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni