MWANASHERIA WACHAMA CHADEMOKRASIA NA MAENDELEO TUNDU LISU |
Timothy
Marko.
Chama cha demokrasia namaendeleo
(CHADEMA) kimelilalamikia kitendo cha jeshi la polisi nchini kuwashikilia wanachama wake tisa
wachama hicho kwatuhuma za kuikosoa serikali na kutowapeleka wanachama hao Mahakamani
kwa kipindi cha wiki mbili .
Wanachama
wanaoshikiliwa jeshi lapolisi nipamoja na Mussa Sikabwe Benjamini Nzogu katika
kituo kikuu cha jeshi lapolisi cha Dar es salaam,wengine ni Shakila
Abdallah,Ignesia Mzega ,David Nicas ,Mdude Nyayali ,Juma Salum,Suleiman Said
pamoja na Jonh Alex wote wakishikiliwa najeshi hilo katika kituo cha oster bay
cha jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mapema hii leo katika makao makuu ya chama hicho yalipo
kinondoni jijini Dar es salaam Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lisu amesema
kuwa kitendo cha kushikiliwa wanachama wa chama chake kwa wiki mbili ni kinyume
nasheria za makosa ya jinai .
‘’Tunalitaka
Jeshi lapolisi litueleze kwanini wamekuwa wakiwa shikilia wanachama wetu kwa
muda wote huo pasipo kufikishwa mahakamani ‘’Alisema Mwanasheria wa Chadema
Tundu Lisu.
Mwanasheria
wa Chadema Lisu alisemakuwa kitendo cha kupinga serikali iliyopo madarakani sio
kosa la jinai kwani sheria inakataza kwa mtu yoyote kudhalilishwa ,kuteswa
kuadhibiwa pasipokupata
idhini ya mahakama kuwa mtu huyo anatakiwa kuteswa .
Alisema
kitendo cha kuteswa na kuadhibiwa najeshi lapolisi nikinyume nasheria za nchi kwani
jeshi lapolisi lipo kikatiba lazima lizingatie misingi ya Kidemokrasia ambapo
kila mtu anayo haki yakutoa maoni juu yaserikali waliyo ichagua .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni