Ijumaa, 9 Septemba 2016

NAIBU KATIBU MKUU AWATAKA VIJANA KUJISHUGHULISHA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA .

Tokeo la picha la ngosi mwihava
NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA RAIS Ngosi Mwihava.



Timothy Marko.
NAIBU Katibu Mkuu ofisi ya Rais nchini Ngosi Mwihava amewataka vijana kujikita katika utunzaji wa Mazingira ilikuweza kuondokana natatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi .

Mwihava aliutoa wito huo wakati akizungumza nawaandishi wa habari jijini Dar es salaam juu yaumuhimu ya utunzaji wa mazingira na kuweka katika uoto wa asili ambapo alisema kuwa shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zina changiwa na shughuli mbalimbali zakibinadamu ambapo mara nyingi zimekuwa zikichangia uharibifu wa mazingira .

‘’Masuala ya mabadiliko ya tabia yanchi yanachangiwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa misitu kwa ajili yamkaa ,hivyo natoa wito kwa vijana kufanya kazi katika kujenga uchumi huku tukizingatia utunzaji wa mazingira kwa vizazi vijavyo ‘’Alisema Naibu Katibu Mkuu Ngosi Mwihava 

Naibu Katibu Mkuu Mwihava alisema kuwa zaidi ya hekta tatu hadi saba za misitu hupotea kutokana nashughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa misitu kwa ajili shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo nabiashara ya mkaa hali inayopelekea uharibifu wa kimazingira .

Alisema kuwa katika kupambana na tatizo hilo ,serikali imejipanga kupambana na uharibifu wa mazingira ikiwemo kuhamasisha upandaji wa miti na uhifadhi wa misitu 
.
‘’Katika kufanikisha suala hili la utunzaji wa mazingira serikali imeweza kupigamarufuku suala zima la matumizi yamifuko ya plastiki kwa kutumia vyombo vya sheria ikiwemo polisi ilikuweza kusimamia sheria mbalimbali za utunzaji wa mazingira ‘’Aliongeza Ngosi Mwihava .



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni