Afisa MWANDAMIZI wa SOKO DSE MARY KINABO |
Timothy
Marko.
KIWANGO cha
mauzo yahisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)kimeshuka kutoka
shilingi bilioni 9 nakuweza kufikia shilingi bilioni moja sawa na asilimia
81kwa wiki hii.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Afisa Mauzo Mwandamizi wa soko hilo
Mary Kinabo amesema hali hiyo imechangiwa kuwepo kwawafanyabishara kufunga
biashara zao kutokana nasikuu ya Idd Alhaji iliyofanyika jumatatu ya wiki
liyopita .
‘’Mauzo
yahisa katika soko letu lahisa la Dar es salaam yameshuka kutoka shilingi
bilioni 9 hadi kufikia shilingi bilioni moja kwa wiki hii,hali iliyochangiwa
kwa wafanyabishara kutofungua biashara zao katika kipindi chasiku kuu ya idd
Alhaji ‘’Alisema Mary Kinabo .
Afisa mauzo
Mwandamizi Kinabo alisema wakati hayo yakitokea ukubwa wamtaji wa soko umeshuka
kwa asilimia 2.79 kutoka shilingi trioni 21.3 kufikia 20.7 wakati huo huo
makapuni yanayo ongoza katika hisa zilizouzwa nakununuliwa nipamoja CRDB (53%) (TBL35%)
huku kampuni Swisport ikishika nafasi yatatu kwa asilimia 3.
Alisema kuwa takwimu katika soko hilo lilionesha
ukubwa wa makapuni yandani umebaki katika kiwango cha awali cha shilingi trioni
8.2 huku sekta ya huduma yakifedha ikionesha kupanda kwa pointi 3.64 baada ya
bei yahisa kupanda katika kaunta DSE kwa asilimia 11.57
‘’Sekta
yahuduma za kibiashara kwa wiki hii imeshuka kwa pointi 4.19 baada ya bei
kupanda kaunta za swisspoti kwa asilimia 0.16’’ Aliongeza Kinabo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni