Jumatatu, 19 Septemba 2016

DSE:IDD ALHAJI YA ATHIRI MAUZO YAHISA

Tokeo la picha la mary kinabo

Afisa MWANDAMIZI wa SOKO DSE MARY KINABO



Timothy Marko.
KIWANGO cha mauzo yahisa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE)kimeshuka kutoka shilingi bilioni 9 nakuweza kufikia shilingi bilioni moja sawa na asilimia 81kwa wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Afisa Mauzo Mwandamizi wa soko hilo Mary Kinabo amesema hali hiyo imechangiwa kuwepo kwawafanyabishara kufunga biashara zao kutokana nasikuu ya Idd Alhaji iliyofanyika jumatatu ya wiki liyopita .

‘’Mauzo yahisa katika soko letu lahisa la Dar es salaam yameshuka kutoka shilingi bilioni 9 hadi kufikia shilingi bilioni moja kwa wiki hii,hali iliyochangiwa kwa wafanyabishara kutofungua biashara zao katika kipindi chasiku kuu ya idd Alhaji ‘’Alisema Mary Kinabo .

Afisa mauzo Mwandamizi Kinabo alisema wakati hayo yakitokea ukubwa wamtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 2.79 kutoka shilingi trioni 21.3 kufikia 20.7 wakati huo huo makapuni yanayo ongoza katika hisa zilizouzwa nakununuliwa nipamoja CRDB (53%) (TBL35%) huku kampuni Swisport ikishika nafasi yatatu kwa asilimia 3.

Alisema  kuwa takwimu katika soko hilo lilionesha ukubwa wa makapuni yandani umebaki katika kiwango cha awali cha shilingi trioni 8.2 huku sekta ya huduma yakifedha ikionesha kupanda kwa pointi 3.64 baada ya bei yahisa kupanda katika kaunta DSE kwa asilimia 11.57 

‘’Sekta yahuduma za kibiashara kwa wiki hii imeshuka kwa pointi 4.19 baada ya bei kupanda kaunta za swisspoti kwa asilimia 0.16’’ Aliongeza Kinabo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni