Jumatano, 1 Juni 2016

WAANDISI NCHINI WAASWA KUTUMIA VIFAA VYA UJENZI VISIVYO HARIBU MAZINGIRA .



Timothy Marko.


WAKALA wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa Vya Ujenzi (NHBRA)imesema kuwa vifaa vingi vinavyotumika katika ujenzi wanyumba nchini husababisha uharibifu wa mazingira ikiwemo uzalishaji wa hewa ya ukaa.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mhandisi wa taasisi hiyo Heri Hatibu amesema kuwa kutokana nautafiti uliofanywa na taasisi ya NHBRA umeweza kubaini kuwa vifaa vinavyotumika katika sekta ya ujenzi huaribu mazingira ikiwemo kuzalisha hewa yaukaa.

‘’Matumizi na namna ya ujenzi wakisasa katika majengo mengi hupelekea kuwepo kwa matumizi makubwa ya uharibifu wa mazingira hii inamanisha kuwa nilazima kuwa na umizania wa matumizi ya matumizi yavifaa vyaujenzi wakisasa pamoja nateknolojia zinzotumika kujenga majengo mbali mbali nchini ‘’Alisema Mhandisi Heri Hatibu .

Mhandisi hatibu alisema kuwa wadau mbalimbali wasekta yaujenzi wanapaswa kuelimishwa kuhusiana nautunzaji wa mazingira ilikuwa namaendeleo endelevu ili kuweza kubaini njia bora yauchomaji wamatofali pasipo kuharibu mazingira .


Alisema kuwa vyombo vyahabari vinavyomchango mkubwa katika kuelimisha wananchi kuhusiana namatumizi ya vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kwenye maeneo yao ili kuweza kupunguza gharama za uhifadhi mazingira.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni