WAANDISI NCHINI WAASWA KUTUMIA VIFAA VYA UJENZI VISIVYO HARIBU MAZINGIRA .
Timothy Marko.
WAKALA wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa Vya
Ujenzi (NHBRA)imesema kuwa vifaa vingi vinavyotumika katika ujenzi wanyumba
nchini husababisha uharibifu wa mazingira ikiwemo uzalishaji wa hewa ya ukaa.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar
es salaam Mhandisi wa taasisi hiyo Heri Hatibu amesema kuwa kutokana nautafiti
uliofanywa na taasisi ya NHBRA umeweza kubaini kuwa vifaa vinavyotumika katika
sekta ya ujenzi huaribu mazingira ikiwemo kuzalisha hewa yaukaa.
‘’Matumizi na namna ya ujenzi wakisasa katika majengo mengi
hupelekea kuwepo kwa matumizi makubwa ya uharibifu wa mazingira hii inamanisha
kuwa nilazima kuwa na umizania wa matumizi ya matumizi yavifaa vyaujenzi
wakisasa pamoja nateknolojia zinzotumika kujenga majengo mbali mbali nchini ‘’Alisema
Mhandisi Heri Hatibu .
Mhandisi hatibu alisema kuwa wadau mbalimbali wasekta
yaujenzi wanapaswa kuelimishwa kuhusiana nautunzaji wa mazingira ilikuwa
namaendeleo endelevu ili kuweza kubaini njia bora yauchomaji wamatofali pasipo
kuharibu mazingira .
Alisema kuwa vyombo vyahabari vinavyomchango mkubwa katika
kuelimisha wananchi kuhusiana namatumizi ya vifaa vya ujenzi vinavyopatikana
kwenye maeneo yao ili kuweza kupunguza gharama za uhifadhi mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni