Msemaji wa WIZARA YAMAMBO YANJE MINDI KASIGA. |
Timothy
Marko.
SERIKALI
imesema kuwa inafuatilia taarifa za Watanzania waliopo katika nchi za uarabuni
nakuangalia taratibu za kuwa rudisha hapa nchini iliwaweze kuendelea nashughuli
za uzalishaji mali hapa nchini.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasilano katika Wizara ya Mambo ya Nje Mindi
Kasiga katika mkutano wa waandishi wa Habari naWizara hiyo, ambapo alisema kuwa
Serikali ipo katika Mipango ya awali ya kuangalia utaratibu wa kuwatengezea
hati za kusafiria kupitia Balozi za Tanzania katika nchi hizo .
‘’Serikali
imewasiliana na Balozi za nchi husika ikiwemo nchi za uarabuni ambapo inadaiwa
kuna watanzania wameshindwa kurudi kutokana na kutokuwa na hati za kusafiria za
kurudi hapa nchini ‘’Alisema Mindi Kasiga .
Katika hatua
nyingine Mkuu huyo wakitengo cha Mawasiliano wa wizara mambo yanje aliwataka Wananchi kuachana na tabia
yakusafirisha bidhaa kwanjia za magendo nabadalayake kufanya biashara kwanjia
za halali .
Alisema kuwa
Nivyema wafanyabishara watanzania wawezeku tumia fursa mbalimbali za soko la
ukanda wa afrika Mashariki kwakuweza kusafirisha bidhaa nakuuza bidhahizo
zilizopo katika ukanda wa afrika mashariki .
‘’Wizara ya
Mambo yanje naushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwajulisha
wafanyabishara wa Tanzania na wananchi kwa ujumla kuweza kutumia fursa za
biashara zinazopatikana katika soko lanchi wanachama wajumuhia ya afrika
Mashariki ‘’Aliongeza Kasiga
Mindi Kasiga
aliongeza kuwa ili mfanyabiashara mdogo aweze kufanyabiashara katika ukanda wa
afrika mashariki anatakiwa kufika kituo chaforodha kilichopo Mpakani akiwa
nabidha yake anayotaka kuiuzakatika ukanda wa afrika mashariki .
Aliongeza
kuwa Mfanyabishara atapatiwa cheti cha uasilia wa bidhaa kilicharahisishwa
ambacho hutolewa na mamlaka yaushuru wa forodha iliyopo mpakani hapo .
‘’Mfanyabiashara
atakiwa kujaza taarifazinzotakiwa kwenye cheti hicho ikwemo jinakamili anuani
nanchi anayotoka namaelezo yabidhaa nathamani ya bidhaa ‘’Alisisitiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni