Alhamisi, 16 Juni 2016

SERIKALI :TUNAENDELEA KUFUATILIA TAARIFA ZA WATANZANIA WALIOZUILIWA UARABUNI .

Msemaji wa WIZARA YAMAMBO YANJE MINDI KASIGA.



Timothy Marko.
SERIKALI imesema kuwa inafuatilia taarifa za Watanzania waliopo katika nchi za uarabuni nakuangalia taratibu za kuwa rudisha hapa nchini iliwaweze kuendelea nashughuli za uzalishaji mali hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasilano katika Wizara ya Mambo ya Nje Mindi Kasiga katika mkutano wa waandishi wa Habari naWizara hiyo, ambapo alisema kuwa Serikali ipo katika Mipango ya awali ya kuangalia utaratibu wa kuwatengezea hati za kusafiria kupitia Balozi za Tanzania katika nchi hizo .

‘’Serikali imewasiliana na Balozi za nchi husika ikiwemo nchi za uarabuni ambapo inadaiwa kuna watanzania wameshindwa kurudi kutokana na kutokuwa na hati za kusafiria za kurudi hapa nchini ‘’Alisema Mindi Kasiga .

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wakitengo cha Mawasiliano wa wizara mambo  yanje aliwataka Wananchi kuachana na tabia yakusafirisha bidhaa kwanjia za magendo nabadalayake kufanya biashara kwanjia za halali .

Alisema kuwa Nivyema wafanyabishara watanzania wawezeku tumia fursa mbalimbali za soko la ukanda wa afrika Mashariki kwakuweza kusafirisha bidhaa nakuuza bidhahizo zilizopo katika ukanda wa afrika mashariki .

‘’Wizara ya Mambo yanje naushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwajulisha wafanyabishara wa Tanzania na wananchi kwa ujumla kuweza kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko lanchi wanachama wajumuhia ya afrika Mashariki ‘’Aliongeza Kasiga 

Mindi Kasiga aliongeza kuwa ili mfanyabiashara mdogo aweze kufanyabiashara katika ukanda wa afrika mashariki anatakiwa kufika kituo chaforodha kilichopo Mpakani akiwa nabidha yake anayotaka kuiuzakatika ukanda wa afrika mashariki .

Aliongeza kuwa Mfanyabishara atapatiwa cheti cha uasilia wa bidhaa kilicharahisishwa ambacho hutolewa na mamlaka yaushuru wa forodha iliyopo mpakani hapo .

‘’Mfanyabiashara atakiwa kujaza taarifazinzotakiwa kwenye cheti hicho ikwemo jinakamili anuani nanchi anayotoka namaelezo yabidhaa nathamani ya bidhaa ‘’Alisisitiza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni