Jumatano, 8 Juni 2016

DSE YAIORODHESHA BENKI YA MUCOBA KATIKA MAKAMPUNI YANAYO UZA HISA ZAKE .

Tokeo la picha la dse

Timothy Marko.
HATIMAYE Soko la hisa la Dar es saalam (DSE)imeiorodhesha Benki ya Mucoba katika makapuni yanayonunua hisa zake kupitia soko hilo ambapo jumla hisa 8,156,423 zimeweza kuuzwa kwa shilingi 250kwa bei yahisa moja .

Akizungumza na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Benki ya Mucoba Beni Mahenge amesema kuwa upatikanaji wahisa hizo zimetokana juhudi mbalimbali za wanahisa kuwekeza katika benki hiyo ambapo benki hiyo ilkuweza kukuza mtaji wake wa shilingi 2,039,105 ,750 .

‘’Kuweza kuorodheshwa kwa benki hii katika orodha yamakampuni yanayouza hisa zake kupitia soko lahisa la Dar es salaam DSE hii imetokana kuwepo kwa sera nzuri za kifedha zinazohamasisha uwazi katika kuwekeza katika kampuni hii ‘’Alisema Mkurugenzi Beni Mahenge .

Mkurugenzi Mahenge alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kuorodheshwa katika soko hilo lahisa la Dar es salaam utawezesha kukuza wigo mpana wa muwekezaji ambaye atanunua katika masoko mbalimbali yamitaji nakuweza kuuza hisa hizo katika masoko mengine yakifedha .

Alisema ilikuweza kununua hisa hizo muwekezaji anaweza kununua hisa zinzouzwa na benki hiyo kwa kupiga namba *150*36# kutoka kwenye orodha yamakampuni yaliyorodheshwa katika soko hilo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni