Jumanne, 7 Juni 2016

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TMA YAWATOA HOFU WANANCHI .


Tokeo la picha la mamlaka ya hali ya hewa tz


Timothy Marko.
MAMLAKA  ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imewatoa hofu wananchi  kuwa mvua zinazoendelea ni zakawaida hazina madhara ambazo huanza mwishoni mwa mwezi Mei na kuishia  Agosti mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa utabiri, Samweli Mbuya, alisema kuwa hali ya mvua hizo zinatokana na hali ya joto katika ukanda wa bahari ya pasifiki kupungua na kusababisha baridi kali inayoambatana na mvua .

‘’Eneo la kusini mwa Afrika kiwango cha joto Kitaweza kupungua ambapo maeneo mengi yatakuwa na joto la wastani ambapo katika nchi yetu tunategemea maeneo katika mikoa ya Mbeya Iringa Pwani na Dar es salaam, ‘’Alisema Mbuya.

 Mbuya alisema kuwa katika maeneo nyanda za juu kusini hayataendelea kuwa nahali yabaridi isipokuwa katika mkoa wa Mbeya .

Alisema lengo lakutoa tahadhari hiyo nikutoa taarifa kwawatumiaji wa usafiri wa maji ikiwemo bahari wanajihusisha nashughuli za usafiri na uvuvi pamoja nautalii ikuweza kupanga mikakati yao kwakuzingatia hali ya hewa nakuweza kujenga uchumi .

 ‘’Hali yajoto ina tofautiana na eneo jingine ambapo tunatarajia kiwango cha joto katika mikoa mingine kinatarajiwa kuwa sentigradi 29 wakati katika mikoa yapwani inatarajiwa kiwango cha joto kitakuwa sentigradi 12C’’Aliongeza Mbuya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni