Jumatano, 8 Juni 2016

BENKI KUU YAISHUKIA BENKI ZA KIBIASHARA .

Tokeo la picha la benki kuu
BENKI KUU YA TANZANIA.


Timothy Marko.
BENKI kuu nchini (BOT)imesemakuwa hali ya kupotea kwashilingi hamisini katika mzunguko imechangiwa na benki zakibishara kutochukua shilingi hizo katika benki kuu ilikuweza kurahisasha mzunguko wa fedha hizo katika soko lakifedha .

Akizungumza na waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa huduma za kibenki katika benki hiyo Marcian Kobello amsema kuwa benki za kibishara huweza kupata wakati mgumu katika kuzibeba sarafu hizo ili ziweze kutumika na wananchi katika mzunguko .

‘’Hali hii ya kupotea kwashilingi hamsini katika mzunguko zimechangiwa na mabenki yakibiashara kuweza kupata wakati mgumu wakuzibeba fedha hizi kwa sababu yakiusalama lakini sisi kama benki kuu hatujazifuta nawala hatuna niahiyo kuziondoa shilingi hamsini katika mzunguko kwani hizi huweza kurahisha katika manunuzi madogo madogo ‘’Alisema Mkurugenzi wahuduma za Kibenki Marcian Kobelo .

Mkurugenzi Kobelo alisema kuwa suala lamatatizo yakukosekana kwakwachenji yamekuwa yakijitokeza siku nyingi hali hiyo inachangiwa namabenki yakibishara kuwa nakiwango cha uchukuaji wasarafu kuanzia shilingi hamsini nakuendelea .

Alisema kuwa hivi karibuni Kumekuwa namalamiko juu ya huduma ya nauli yamabasi yamwendo kasi alimamarufu “DART”Kukosa chenji yashilingi hamsini kutokana na madai ya benki kuu hiyo kutoruhusu fedha hizo kutkokuwepo kwenye mzunguko ambapo mkurugenzi huyo alisema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote .

‘’DART kama wanataka chenji waje wachukue chenji hizo kwa kuomba order maalum kutoka benki yakibiashara ya  NMB ya kuombauhitaji wachenji hizo hatakama shilingi milioni 10 tutawapa kwani shilingi hamsini tunazo nyingi  hivyo tutajaribu leo,au hatakesho kuwasiliana NMB au NBC Ilikuweza kutatua suala hili ‘’Aliongeza Mkurugenzi KOBELO.

Kobelo  aliongeza kuwa lengo lakutoziondoa shilingi hamsini katika mzunguko nikuweza kurahisisha mihamala midogo midogo ikiwemo sokoni katika kuweza kununua bidhaa pasipokuwa na matatizo yoyote .

Aliongeza Noti za miatano zinatoka katika mzunguko hii imechangiwa na gharama za kupriti fedha hizo kwani fedha hizozimeonekana ni nyingi katika mzunguko wa fedha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni