Timothy
Marko.
CHAMA cha
Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi nchini(COTWU(T)kimewasimamisha
Uwanachama wafanyakazi wanne wataasisi hiyo baada yakuhusika natuhuma
za ubadhilifu wa shilingi milioni 120 za chama hicho.
Akizungumza
na wandishi wa habari mapema hiileo jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Idrisa Washington amesema kuwa
watumishi waliosimamishwa kwatuhuma za ubadilifu nipamoja na aliyekuwa
mwenyekiti wa tasisi hiyo nchini Alfred Lugendo ,Katibu mkuu Mathias Mjema
,Kaimu Katibu mkuu Moses Matonelo pamoja
na Muhasibu wa chama hicho Janeth Senga.
‘’Kufuatia
kikao cha ripoti ya ukaguzi wa fedha ya kampuni ya (H.H Marine )nakubaini wizi
na upotevu washilingi milioni 120ndani yachama uliofanywa naviongozi hao
waliosimamishwa ,kufuatia matokeo yaripoti hiyo itapelekwa kwenye Mkutano Mkuu
wa COTWU ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu kwajili ya kuamua
hatima ya wanachama hawa ‘’ Alisema Kaimu Mwenyekiti Idrisa Washington.
Kaimu
Mwenyekiti Washington alisema kuwa kufuatia sakata hilo chama hicho kimepanga
kukutana naviongoziwamatawi yote nchini wa chama hicho kuanzia mwezi julai
ambapo agenda yakikao hicho nijuu ya muundo mpya wa chama hicho unalenga
maslahi ya wanachama wachama hicho.
Alisema kuwa
kufuatia kusimamishwa kwa wafanyakazi
hao chama hicho kimepanga kufanya uchaguzi wa viongozi wachama hicho juni mosi
mwaka huu ambapo uchaguzi huo utajumuisha kanda zote za taasisi hiyo nchini .
‘’Uchaguzi
huu umepangwa kufanyika agosti 29hadi 31 mkoani Dodoma ninatoa rai kwa waajiri
wote waweze kufuata taratibu kwa mujibu washeria ili kuweza kuepusha migogoro isiyo
ya lazima ‘’Aliongeza Kaimu Mwenyekiti Idrisa Washitongton.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni