Alhamisi, 11 Februari 2016

SERIKALI TUTAENDELEA KUSAIDIA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Naibuwaziri wa fedha na uchumi Ashatu KIJAJI  akiteta jambo na Mkurugenzi wa mfuko wa pesheni PPF Wiliam Erio mapema hii leo jijini Dar es salaam




Timothy Marko.

SERIKALI imesemakuwa itaendelea kusaidia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini ilkuweza kutoa huduma kwa watumishi wa serikali katika kuwakikishia wananchi wa nanufaika namifuko hiyo ya hifadhi ya jamii nchini .

Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mfuko wa pesheni wa PPF Naibu Waziri wa fedha na uchumi ASHATU KIJAJI amesema kuwa katika kipindi kinachoishia mwaka jana jumla ya shilingi trioni moja ziliweza kupatikana kutokana namifuko ya hifadhi ya jamii .

‘’PPF Mmeweza kutoa mikopo ya shilingi bilioni 91.34 kwa wanachama wenu ni jambo zuri lakini ,natoa rai kwenu muweze kuwaangalia wakulima ilikuweza kunufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii ‘’Alisema Naibu waziri Ashatu Kijaji.

Naibu waziri wa fedha na uchumi Ashatu Kijaji alisema kuwa nivyema mifuko ya hifadhi yajamii iwezekupanua matawi yake katika maeneo ya vijijini.  

Alisema kuwa nivyema waajiri wawasilishe michango ya watumishi wao kwa wakati kwani kutofikisha michango hiyo kwenye mifuko hiyo nikinyume cha sheria za utumishi wauma .

‘’Kwa wale wanao kiuka kurejesha michango ya waajiriwa kwa wakati  wachukuliwe hatua za kisheria’’ aliongeza  Naibu WAZIRI Ashatu .

Mkurungenzi wa PPF Wiliam erio amesema kuwa niwajibu waserikali kuweza kuisaidia mifuko hiyo ili iweze kujiendesha .

Alisema serikali inawajibukuwaelimisha waajiri kuresha michango yaw a tumishi kwa wakati . 

‘’Kuna kasi kubwa yaulimishaji kwa wanachama ikiwemo mamlaka inayosimamia mifuko hii ya ifadhi juu yaureshaji wamichango kwa wakati ‘’Alisema Wiliam Erio.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni