KAMISHINA Uhamiaji KANDA Dar es salaam Jonh Msumule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani )mapema hii leo |
Timothy Marko.
WIZARA
yamambo ya ndanikitengo cha idara ya uhamiaji ina washikilia Kashama Alan
Mulumba (39) Mwenabantu Kibyakibya Michael (35)Raia wa jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo kwa tuhuma za kuishi nchini bila kibali .
Raia hao wa
nchini kongo ambao pia niwanamziki wa bendi ya kalunde walikamatwa February 10 mwaka huu katika
manispaa ya kinondoni wakiishi bila kuwa nakibali chakuishi nchini .
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Kamishina Idara
ya uhamiaji mkoa wa Dar es salaam JONH
Msumule amesema kuwa kutokana nasheria za nchi ni kosa kuajiri mtu yoyote
ambaye si raia ambaye hana kibali cha kuishi nchini .
‘’Tuna
mshililia mMiliki wa bendi ya Kalunde
Geofrey Manambilimbi kwa kuwa nawafanyakazi ambao si raia watanzania na hawana
kibali cha kuishi nchini kwa mujibu wa sheria ‘’Alisema Naibu Kamishina JONH
Msumule .
Baadhi ya wanamziki wakalunde BAND |
Alisema kuwa
sambamba nakuwashikilia raia wa nchini Kongo
ambao ni wanamziki wakalunde band kwatuhuma za kutokuwa nakibali pia
jeshi hilo ,linawashikilia Asma Mkeyenge (26) mkazi wa Tandika ,Nyamizi Kambuga
(31)mkazi wa mbagala Misioni kwatuhuma za usafirishaji wa binadamu
‘’Watuhumiwa
hawa wote watafikishwa mahakamani kesho kujibu mashitaka yakutoishi bila kibali
cha kuishi nchini watanzania acheni kuishi na wahamijia haramu nihatari kabisa
kwa maisha yenu ‘’Aliongeza Kamishina
Msumule .
Raia wa
nchini kongo ambaye anatuhumiwa kuishi bila kibali nchini Kibyabya Michel(26)
aliwaambia waandishi wa habari kuwa amekuja nchini Tanzania ili aweze kufanya
kazi yamuziki ili aweze kutibiwa macho ili aweze kurudi kwao nchini kongo.
‘’nimekuja
hapa nchini Tanzania iliniweze kujishughulisha na muziki kwani hali yangu ya
afya nimbaya nina umwa macho kwa hiyo nimekuja hapa kuweza kupata fedha ili
niweze kutibiwa ikiwezekana nirudi zangu nchini kongo sitaki kukaa hapa ,sitaki
kukaa jela sija zoea maisha yajela ‘’Alisema .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni