Jumatano, 10 Februari 2016

WAZIRI WA AFYA :OFISI YA MKEMIA MKUU INAO MCHANGO MKUBWA KATIKA KUHARAKISHA UCHUNGUZI WA MAKOSA YA JINAI



Timothy Marko.
KATIKA Kuhakikisha afya na usalama wa watanzania wizara ya afya imesema kuwa inatambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi ya mkemia mkuu kwa kutekeleza uchunguzi wakitalamu wamakosa mbalimbali yakijinai nchini .

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari la Huduma za dharura lakituo cha taifa chakuratibu matukio ya sumu jijini Dar es salam waziri wa afya ,Maendeleo ya jamii,jinsia watoto na wazee Ummy Mwalimu amesema kuwa ili kuharakisha uchunguzi wa makosa ya jinai nchini taasisi hiyo inayo mchango muhimu katika kuhakikisha haki katika vyombo vyasheria inapatikana kwakutoa ushauri wakitalam.

‘’ILI hii taasisi hii iweze iendelee kufanya kazi zake kwa ufanisi Zaidi uwepo wamiundo mbinu kama vile ikiwemo mitambo vitendea kazi kama vile magari na majengo bora nisuala linalotakiwa kuwekewa kipaumbele ‘’Alisema Waziri wa afya Ummy MWALIMU 

WAZIRI UMMY alisema kuwa taasisi hiyo inayo majukumu ya uchunguzi wa sampuli zinzohusiana na makosa ya jinai kama vile dawa za kulevya ,utambuzi wasumu ,watu wanao jihusisha na uhalifu ,utambuzi wa vinasaba 

Alisema kuwa unzishwaji wa kanzi data ya watanzania itawezesha kukabiliana navitendo vyakihalifu nawahalifuhasa walewahalifu wanaojirudia makossa .  .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni