Timothy Marko .
WAKATI TANZANIA Ikielekea kuadhimisha siku ya kupinga ukeketaji duniani zaidi ya
asilimia 15 ya wanawake nchini waliopo nyanda za juu kasikazini wamefanyiwa
vitendo vya ukeketaji huku mkoa wa manyara ukiwa unaongoza kwa vitendo hivyo .
Katibu MKUU WA AFYA,JINSIA MAENDEO YAJAMII ,JINSIA NA WATOTO |
Akitoa takwimu
hizo mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya afya
,maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto SIHABA NKINGA amesema kuwa mbali na
Tanzania kuridhidhia mikataba mbalimbali ya haki za mtoto kimataifa lakini
kumekuwa namila nadesturi zinazokwamisha utokomezaji wa vitendo hivyo.
‘’Ukeketaji
umekuwa ukijiridhihirisha katika sura mbambali ikiwemo baadhi yamakabila
kuhalalisha vitendo vya ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi za kabila
husika ‘’Alisema Katibu mkuu Sihaba Nkinga.
Katibu mkuu
SIHABA alisema kuwa mikoa ya Dodoma, Arusha ,singida ndio inayoongoza
kwakuhalalisha vitendo vya ukeketaji licha yaserikali kuridhia mikataba
mbalimbali yakimataifa .
Alisema
Mikataba yakimataifa iliyosaini na nchi ya Tanzania nipamoja na Mkataba wa haki
yamtoto wa mwaka 1989,Mkataba wakuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake 1979,Mkataba
wa afrika wa Haki za binadamu nahaki za watu 1982 .
‘’Kwamujibu
wa ibara 9(4)yakatiba inaeleza kuwa sheria yoyote ,mila desturi au uamuzi ambao
hautawiana kwenda sambamba na masharti ya katiba utakuwa batili .’’Aliongeza
KATIBU MKUU SIHABA NKINGA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni