Ijumaa, 5 Februari 2016

MILA NA DESTURI ZA MAKABILA ZAWA KIZINGITI KWA TANZANIA KATIKA KUTOMEZA UKEKETAJI.



Timothy Marko .
WAKATI TANZANIA Ikielekea kuadhimisha siku ya kupinga ukeketaji duniani zaidi ya asilimia 15 ya wanawake nchini waliopo nyanda za juu kasikazini wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji huku mkoa wa manyara ukiwa unaongoza kwa vitendo hivyo .

Katibu MKUU WA AFYA,JINSIA MAENDEO YAJAMII ,JINSIA NA WATOTO

Akitoa takwimu hizo mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto SIHABA NKINGA amesema kuwa mbali na Tanzania kuridhidhia mikataba mbalimbali ya haki za mtoto kimataifa lakini kumekuwa namila nadesturi zinazokwamisha utokomezaji wa vitendo hivyo.

‘’Ukeketaji umekuwa ukijiridhihirisha katika sura mbambali ikiwemo baadhi yamakabila kuhalalisha vitendo vya ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi za kabila husika ‘’Alisema Katibu mkuu Sihaba Nkinga.

Katibu mkuu SIHABA alisema kuwa mikoa ya Dodoma, Arusha ,singida ndio inayoongoza kwakuhalalisha vitendo vya ukeketaji licha yaserikali kuridhia mikataba mbalimbali yakimataifa .

Alisema Mikataba yakimataifa iliyosaini na nchi ya Tanzania nipamoja na Mkataba wa haki yamtoto wa mwaka 1989,Mkataba wakuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake 1979,Mkataba wa afrika wa Haki za binadamu nahaki za watu 1982 .
‘’Kwamujibu wa ibara 9(4)yakatiba inaeleza kuwa sheria yoyote ,mila desturi au uamuzi ambao hautawiana kwenda sambamba na masharti ya katiba utakuwa batili .’’Aliongeza KATIBU MKUU SIHABA NKINGA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni