Timothy Marko.
Wizara ya
nishati na madini imekanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la mtanzania la leo
lililoandika kichwa chahabari ‘’Harufu
ya jipu mradi wa umeme’’ ambao uligharimu shilingi trioni 1.6 fedha ambazo
zilipatikana kutokana na ubia wa serikali ya japan pamoja na Tanzania .
Akitoa
ufafanuzi kuhusiana natuhuma za ufisadi katika miradi ya umeme iliyofadhiliwa
naserikali ya japan Afisa mawasilino wa Wizara hiyo Badra Masoud amesema kuwa
Serikali iliingia makubaliano na serikali ya japan ya mkopo wa mashariti na fuu
wa dola za kimarekani milioni 292 kwa ajili ya kuzalisha umeme wa megawati 240
.
‘’Mradi huu
wa kuzalisha umeme unafadhiliwa na kampuni ya SUMITOMO ya nchini Japan kama mkandarasi nasivyo ilivyo eleza gazeti hili
lamtanzania kuwa EPC contractor na wala
serikali ya Tanzania kuwa kama mbia kwa mujibu wa gazeti hili ‘’Alisema Badra
Masoud .
Afisa
Mawasiliano Badra alisema kuwa Katika mradi huo unamilikiwa nashirika la
tanesco kwa asilimia miamoja na hakuna muwekezaji mwingine aliingia ubia katika
mradi huo wakuzalisha umeme .
Alisema kuwa
taarifa zilizotolewa na chombo hicho cha habari si zakweli nakuwa kampuni ya SUMITOMO pamoja na serikali
ziliwekeana ubia kwa asilimia 40 kwa upande waserikali huku kampuni hiyo
ikimili kwa ubia wasilimia 60 .
‘’Mwandishi
wa habari hii ameudanganya umma kwamba mradi uliozinduliwa na Rais Jakaya
KIKWETE ukweli kwamba mradi huu bado haujazinduliwa bado lakini upokatika
maandalizi ya kuwekewa jiwe la msingi unaendelea ‘’Aliongeza Badra .
Badra
aliongeza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 740 na
sivyo ilivyoripotiwa nachombo hicho cha habari kuwa trioni 1.6 ziweza
kugharamia mradi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni