Na Timothy
Marko.
JUMLA Shilingi trilioni 71.7 zimeweza
kupatikana katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka jana sawa na
ongezeko la pato la taifa la asilimia 6.9 ikilinganishwa pato la taifa la
nchini Kenya la 5.8.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii
leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Ofisi ya Takwimu nchini Albina Chuwa
amesema kuwa ongezeko hilo la pato la taifa limetokana na kuongezeka kwa mauzo
ya dhahabu na almasi na madini mengine pamoja na kukua kwa sekta ya utalii
nchini .
‘’Katika kipindi cha robo tatu ya mwaka jana
viashiria vyakiuchumi vimeonesha kutoyumba kwa uchumi ambapo thamani ya mauzo
ya bidhaa na huduma nje yanchi imeongezeka kwa asilimia 3.3 bidhaa
zilizochangiwa ni pamoja na dhahabu na almasi na madini mengine ‘’AlisemaAlbina
chuwa .
Chuwa alisema kuwa, thamani ya bidhaa na
huduma zilizoagizwa kutoka nje ziliweza kupungua katika kipindi cha mwezi
Septemba na kuweza kufikia asilimia 0.58.
Alisema sekta ya kilimo iliweza kukua kwa
asilimia 2.6 kwa mwaka jana ikilinganishwa 3.1 katika kipindi cha mwaka 2014.
‘’Shughuli ndogo ya uzalishaji mazao ya kilimo
ikiwemo zao la mahindi limeweza kuchangia asilimia 23 katika pato la taifa
ikilinganishwa kipindi cha mwaka jana ambapo jumla ya tani 2,148000 ziliweza
kuzalishwa ‘’Aliongeza CHUWA .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni