Alhamisi, 14 Januari 2016

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKANUSHA MADAI YA KUWEPO KWA RUSHWA KATIKA MIRADI YA UMEME .



Timothy Marko.
Wizara ya nishati na madini imekanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la mtanzania la leo lililoandika kichwa chahabari ‘’Harufu ya jipu mradi wa umeme’’ ambao uligharimu shilingi trioni 1.6 fedha ambazo zilipatikana kutokana na ubia wa serikali ya japan pamoja na Tanzania .

Akitoa ufafanuzi kuhusiana natuhuma za ufisadi katika miradi ya umeme iliyofadhiliwa naserikali ya japan Afisa mawasilino wa Wizara hiyo Badra Masoud amesema kuwa Serikali iliingia makubaliano na serikali ya japan ya mkopo wa mashariti na fuu wa dola za kimarekani milioni 292 kwa ajili ya kuzalisha umeme wa megawati 240 .

‘’Mradi huu wa kuzalisha umeme unafadhiliwa na kampuni ya SUMITOMO ya nchini Japan kama mkandarasi nasivyo ilivyo eleza gazeti hili lamtanzania kuwa EPC contractor   na wala serikali ya Tanzania kuwa kama mbia kwa mujibu wa gazeti hili ‘’Alisema Badra Masoud .

Afisa Mawasiliano Badra alisema kuwa Katika mradi huo unamilikiwa nashirika la tanesco kwa asilimia miamoja na hakuna muwekezaji mwingine aliingia ubia katika mradi huo wakuzalisha umeme .

Alisema kuwa taarifa zilizotolewa na chombo hicho cha habari si zakweli  nakuwa kampuni ya SUMITOMO pamoja na serikali ziliwekeana ubia kwa asilimia 40 kwa upande waserikali huku kampuni hiyo ikimili kwa ubia wasilimia 60 .

‘’Mwandishi wa habari hii ameudanganya umma kwamba mradi uliozinduliwa na Rais Jakaya KIKWETE ukweli kwamba mradi huu bado haujazinduliwa bado lakini upokatika maandalizi ya kuwekewa jiwe la msingi unaendelea ‘’Aliongeza Badra .

Badra aliongeza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 740 na sivyo ilivyoripotiwa nachombo hicho cha habari kuwa trioni 1.6 ziweza kugharamia mradi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni