Timothy Marko.
KIWANGO cha mauzo ya hisa katika soko la Dar es
salaam(DSE ) kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 1hadi kufikia shilingi
bilioni 5 kwa wiki hii.
Ongezeko
hilo la asilimia sabini natano limetokana baadhi ya makampuni yandani kuongeza kiwango cha mauzo ya hisa
katika soko hilo .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini mapema hii leo ,Meneja Mauzo na Biashara Patrick
Mususa amesema kuwa sambamba naongezeko la makapuni ya ndani kuongeza idadi ya
mauzo ya hisakwenye soko hilo ,pia soko hilo la hisa la jijini Dar es salaam
limeweza kuongeza huduma zake ikiwemo kutoa bidhaa zake zinazotokana na hisa
hali iliyochangia kuongezeka kwa uchumi katika soko hilo .
‘’Baadhi ya
makampuni ya ndani yameongeza mauzo katika soko la hisa la Dar es salaam
(DSE)kwa mwaka huu hali hii imechangia sana katika kuongeza kiwango cha mauzo
kutoka shilingi bilioni 1hadi kufikia bilioni 5hali hii imechangiwa na ongezeko
la bidhaa katika soko la hisa nakuweza kuongezeka kwa uchumi ‘’Alisema Patrick Mususa
.
Meneja Mauzo
Patrick Mususa alisema kuwa kiwango cha mtaji katika soko kimeweza kufikia
trioni 21.6 kutoka trioni 21.5 nakuweza kusababisha sekta yaviwanda kupungua
kwa asilimia35 na wakati huo sekta ya kibenki imeweza kupungua kwa asilimia 32.
Alisema kuwa
katika kipindi cha mwezi January mwaka huu makapuni mengi yameweza kuongeza
hati fungani ikilinganishwa na mwaka jana .
‘’Makampuni
yanayo ongoza kwa uuzwaji wa hisa katika soko la hisa kwa wiki hii ni pamoja
CRDB pamoja na TBL ‘’Aliongeza Mususa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni