Alhamisi, 4 Septemba 2014

MWANAFUNZI WA SHULE YAMSINGI ATIWA HATIANI KWATUHUMA ZA KUWAIBIA ABIRIA JIJINI.


Timothy Marko.
MWANAFUNZI wa shule ya msingi ya upendo  Iren Kingu (11)anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaibia abiria  fedha katika mabasi maarufu kama daladala ambapo  mwanafunzi huyo hupanda  magari hayo aina yadaladala nakwenda katika maeneo yaposta yaliyopo jijini hapa nakuanza kufanya upekuzi  kwenye mikoba ya wasafiri wanaotumia daladala hizo .

Akizungumza nawaandshi wa habari shuhuda wa tukio hilo wigan michael amesema kuwa mwanafunzi huyo amekuwa akipewa kiasi cha shilingi minane nawazazi wake lakini mwanafunzi huyo hudai kuwa fedha hizo hazimtoshi .

‘’Mwanafunzi huyu anasoma huko mbezi lakini safari zake zinaleta utata mara utaweza kumuona katika maeneo ya karikoo na saa nyingine katika maeneo yaposta alikuwa akipekuwa mikoba ya watu na kuiba fedha katika mikoba hiyo huu ndio ulikuwa mtindo wake ‘’Alisema Shuhuda watukio hilo Wigan Michael .
Katika hatua nyingine mwalimu wa shulehiyo YUSSUPH ZANNY alithibititisha kuwa mwanafunzi huyo nikweli anasoma katika shule hiyo nakusitiza kuwa kwapindi hicho cha mahojiano kwa njia yasimu asingeweza kuongea na mwandishi .
‘’sipo katika nafasi nzuri yakuongea na mwandishi ninaomba mtanipigia baadaye ‘’alisema mwalimu wa shule hiyo ya msingi upendo .
Askari wajeshi lapolisi kropo Kalenzo alisema kuwa walipata taarifa ya mwana funzihuyo baada wasamalia wema kulipigia jeshi lapolisi kuwa kuna mwanafunzi ambaye amevaa nguo za shule ndipo jeshi hilo likaanza kufanya upelelezi nahatimaye mtoto huyo amepelekwa kwenye dawati lajinsia kwaupelelezi zaidi .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni