Jumatano, 27 Agosti 2014

SEKRETARIETI YA AJIRA YA WATAKA WANAOTAFUTA KAZI KUFANYA UHAKIKI WA MAJINA KWENYE VYETI VYAO MAHAKAMANI .

Timothy Marko.
Katika kuhakikisha Sekta ya ajira inakuwa naubora unaotakiwa kwa kuhakiki viwango mbali mbali vya waajiriwa nanao ajiriwa katika taasisi pamoja namashirika ya umma serikali kuptitia seketarieti ya ajira nchini ime wataka wahitimu walio maliza vyuo pamoja nasekondari nje ya nchi kupeleka vyeti vyao ili viweze kuhakikiwa  natume ya vyuo vikuu (TCU) Pamoja na baraza la usimamizi wa elimu ya vyuo vya ufundi  (Nacte) na katika ngazi yasekondari NECTA.
Akizungumza jijini leo,Msemaji wa Sekretarieti ya ajira nchini Riziki Abraham amesema kuwa mamala hizo ndizo zenye dhamana kuthibitisha amakuwasilisha taarifa za muhusika analiye potelewa na vyeti katika ofisi hiyo.
‘’Mamlaka hizo ndizo zenye dhamana kuthibitisha ama kuwasili sha taarifa za muhusika aliyepotelewa na vyeti katika sekretarieti ya ajira kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini na sio mtu aliyepotelewa kuwasilisha utambulisho wa matokeo ama nyaraka mbalimbali anapoomba kazi ‘’Alisema Riziki Abraham.
Riziki Abraham alisemakuwa sekretarieti ya ajira inawataka wale wote wenye majina yao tofauti katika vyeti kwenda mahakamani kwakamishina wakiapo ilkuweza kupata Affidavity Kwamujibu wa sheria .
Alisema kuwa tabia yakubadilisha majina kienyeji inaweza kuwa sababishia kuwanyima haki zao wakati mwingine kwakufanya hivyo kutawasaidia kuthibitisha uhalali wa utofauti ya majina yanayo tambulika kisheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni