Timothy Marko
KATIKA
kukabiliana na tatizo la Ndoa za utotoni Serikali imesema kuwa inaifanyia mbadilko ya sheria ya mwaka 1971 katika
mchakato wa kupata katiba mpya ilkuondokana sheria zinzoruhusu mtoto mwenye
chini ya miaka 15 kuweza kuolewa ambapo sheria hiyo inakinzana na sheria
inayotafurusiri kuwa mtu mwenye umri wa miaka 18 ndiye anayeruhusiwa kisheria
kuoa au kuolewa .
Akizungumza
jijini leo Katibu wa wizara ya jinsia na
watoto Anna maembe amesemakuwa katika
takwimu zilizopo inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwepo kwandoa za
utotoni ikilinganishwa nanchi nyingine za bara la afrika .
‘’Takwimu
zinaonesha kuwa Tanzania ina tatizo kubwa la ndoa za utotoni ndio maana
tumeonelea tulianze kulipinga swala hili ‘’Alisema Anna Maembe
Maembe Alisema kuwa kwakushirikiana serikali na wadau mbalimbali wakiwemo taasisi ya
TAMWA ina weza kulitokome za tatizo landoa za utotoni endapo jitihada
mbalimbali zitaundwa nakushirikiana katika kutoa michango mbalimbali ya mawazo
yatakayoweza kuratibu sera pamoja nasheria ilkuweza kulitekeleza suala hilo.
Alisema
katika kuondokana natatizo la ndoa za utotoni pia vyombo vya habari vinavyo wajibu
mkubwa wa kukemea na kuonya juu ya masuala malimbali ikiwemo kuwa wafichua wa
wahalifu wanao kiuka sheria ya mtoto ikiwemo kuolewa katika umri mdogo .
‘’Vyombo
vya habari vinanguvu kwahiyo ninawaomba waandishi wa habari muweze kukemea
suala hili kwa kuandika habari zinzohusu vitendo vya unyanyasaji wawatoto
ikiwemo ndoa za utotoni ‘’Aliongeza Katibu wa wizara hiyo Anna Maembe .
Katika
hatua nyingine Muwakilishi mkazi wa shilika laumoja wa mataifa linahusiana na
idadi ya watu duniani UNPA Natalia Kanem amesema kuwa kati ya wasichana watano
waliopo walio chini ya miaka 18 barani afrika wawili hukumbwa na tatizo la ndoa
za utotoni .
Natalia
Kanen alisema kuwa wasichana hao ambao sawa nasilimia 42 ya watoto wakike
waishio katika bara la afrika ambapo alizitaja sababu zinazo sababisha watoto
hao kuolewa mapema nipamoja na kutafuta utajiri kwa jamii za kiafrika .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni