Timothy Marko.
KITUO cha
sheria nahaki za binadamu kimelitaka bunge lakatiba pamoja na serikali
kuheshimu uhuru wa maoni na kupokea habari kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya
muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ilkuepusha kutoa kauli ambazo zitakuwa
chanzo cha kuzorotesha umoja na amani katika nchi .
Akizungumza
jijini leo na waandishi wa habari Mkurugenz I wa kituo hicho Helen Kijo Bisimba
amesema kuwa ni vyema wananchi wa kapewa uhuru wakujadili hatima ya taifa lao
kupitia mchakato wa katiba mpya ikiwemo wajumbe wabunge hilo kuheshimu mawazo
ya wananchi yaliyopo kwenye rasmu yapili ya katiba .
‘’Tunapendekeza
bunge la katiba kusitisha mjadala wa sura zilizo salia na kufanya kila
liwezekanalo kumaliza mgogoro kati yao ili majadiliano ya kiendelea kuwepo na uhakika
wa kufikia kupiga kura na mapendekezo ya katiba mpya yawe na uhalali wa
kisheria na kisiasa ‘’Alisema Hellen kijo Bismba .
Hellen
Bisimba alisema kuwa kufuatia kupigwa marufuku kwa makongamano pamoja na
mikutano ya hadhara na mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa madai ya kuepuka kuwa
changanya wajumbe wabunge lakatiba katazo hilo limekiuka sheria ibara ya 18 na
21 (2)ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambazo zinatoa haki kwa
kila mwananchi kupata habari pia uhuru wa kushiriki wa maswala yanayomhusu na
kuathiri jamii yake .
Alisema
Taasisi hiyo inatambua kuwa kila mwananchi anayo haki ya kujadili kuuliza,kuhabarisha
kuhusu katiba nakusisitza kuwa taasisi hiyo imeshuhudia kufanyika kwa midahalo
huru ya uuma ikiwa na manufaa makubwa
kwa kuwa kumbusha wananchi katika mchakato wa katiba.
‘’kituo cha
sheria na haki za binadamu tumesikitishwa na tunapiga vita vikali mapendekezo
yaliyotolewa na mwenye kiti wa bunge lakatiba Samweli Sitta mnamo tarehe 5
agosti mwaka huu yenye dhana ya kukerwa na midahalo ina yoendelea ‘’Aliongeza
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helleni kijoBisimba .
KATIKA hatua
nyingine chama cha mapinduzi CCM kime pinga vikali hatua ya Juu ya mwenyekiti
wa Tume ya marekebisho yakatiba kushukia Rais Jakaya kikwete kuwa kupendekeza
muundo wa serikali mbili badala ya serikali tatu na kusisitiza kuwa Rais JaKAYA
KIKWETE alitoa maoni kama mtu mwingine hivyo maoni ya Rais yaheshimiwe .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni