Alhamisi, 7 Agosti 2014

KITUOCHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHA WATAKA WAJUMBE WA BUNGE LAKATIBA KUHESHIMU MAONI YA WANANCHI

Timothy Marko.
KITUO cha sheria nahaki za binadamu kimelitaka bunge lakatiba pamoja na serikali kuheshimu uhuru wa maoni na kupokea habari kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ilkuepusha kutoa kauli ambazo zitakuwa chanzo cha kuzorotesha umoja na amani katika nchi .
Akizungumza jijini leo na waandishi wa habari Mkurugenz I wa kituo hicho Helen Kijo Bisimba amesema kuwa ni vyema wananchi wa kapewa uhuru wakujadili hatima ya taifa lao kupitia mchakato wa katiba mpya ikiwemo wajumbe wabunge hilo kuheshimu mawazo ya wananchi yaliyopo kwenye rasmu yapili ya katiba .

‘’Tunapendekeza bunge la katiba kusitisha mjadala wa sura zilizo salia na kufanya kila liwezekanalo kumaliza mgogoro kati yao ili majadiliano ya kiendelea kuwepo na uhakika wa kufikia kupiga kura na mapendekezo ya katiba mpya yawe na uhalali wa kisheria na kisiasa ‘’Alisema Hellen kijo Bismba .
Hellen Bisimba alisema kuwa kufuatia kupigwa marufuku kwa makongamano pamoja na mikutano ya hadhara na mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa madai ya kuepuka kuwa changanya wajumbe wabunge lakatiba katazo hilo limekiuka sheria ibara ya 18 na 21 (2)ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambazo zinatoa haki kwa kila mwananchi kupata habari pia uhuru wa kushiriki wa maswala yanayomhusu na kuathiri jamii yake .
Alisema Taasisi hiyo inatambua kuwa kila mwananchi anayo haki ya kujadili kuuliza,kuhabarisha kuhusu katiba nakusisitza kuwa taasisi hiyo imeshuhudia kufanyika kwa midahalo huru ya uuma ikiwa na manufaa makubwa  kwa kuwa kumbusha wananchi katika mchakato wa katiba.
‘’kituo cha sheria na haki za binadamu tumesikitishwa na tunapiga vita vikali mapendekezo yaliyotolewa na mwenye kiti wa bunge lakatiba Samweli Sitta mnamo tarehe 5 agosti mwaka huu yenye dhana ya kukerwa na midahalo ina yoendelea ‘’Aliongeza Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helleni kijoBisimba .
KATIKA hatua nyingine chama cha mapinduzi CCM kime pinga vikali hatua ya Juu ya mwenyekiti wa Tume ya marekebisho yakatiba kushukia Rais Jakaya kikwete kuwa kupendekeza muundo wa serikali mbili badala ya serikali tatu na kusisitiza kuwa Rais JaKAYA KIKWETE alitoa maoni kama mtu mwingine hivyo maoni ya Rais yaheshimiwe .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni