Timothy Marko
KUFUATIA msako mkali uliotangazwa najeshi lapolisi jijini Dar es salam wa kuwakamata Majambazi waliohusika katika kifo cha aliyekuwa Mtawa wa kanisa katoliki Sista Clesencia Kapuri (50)juni 23 mwaka huu huko Ubungo Kibangu hatimaye leo jeshi hilo limewashawatia nguvu ni watuhumiwa walikuwa wakikusika na tukio hilo la uhalifu.
Akizungumza jijini leo ,kamishina wa Polisi wa kanda Maalumu jiji Dar es salaam Sulemani Kova amesema kuwa watuhumiwa wanane walio kamatwa kuhusika na tukio hilo kati yao wawili wamehusishwa moja kwa moja na mauwaji yaliyekuwa mtawa huko ubungo kibangu katika kanisa la katoliki parokia ya makoka .
‘’Wawili kati yawatuhumiwa hao wanane wamehusishwa moja kwa moja natukio lakuuwawa kwa mtawa ambao wa wakwanza ni Manase Ogenyeka maarufu kama ‘’Mjeshi’’ (35)mkazi wa tabata Changombe ambaye pia ni mwendesha Boda boda wapili ni Hamisi Isimail Shabani ambaye ni mfanyabiashara napia ni mkazi wa Magomeni Mwembe chai.’’Alisema Suleiman KOVa.
Kamanda Kova alisema majambazi hao hatari licha ya kuhusishwa na tukio hilo lakifo la aliyekuwa mtawa wa kanisa katoliki parokia ya nakupora shilingi miloni ishirini kutoka kwa mtawa huyo anaishi maeneo ya makoka pia majambazi hao walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwatuhuma za kufanya uporaji wa benki ya Barcrays tawi lakinondoni.
Alisema kuwa katika tukio hilo mamilioni yafedha yaliibiwa kabla ya jambazi huyo ambaye alijukana kama ‘’mjeshi ‘’ alkikutwa akiendesha pikipiki nakuumbeba jambazi mwenzake wakiwa nafuko lililojaa mamiloni yafedha nakutoroka na fedha hizo ambapo jambazi aliyejulikana kwa jina Hamis Ismail SHABANI ndie kiongozi wa tukio hilo la uhalifu.
‘’Jeshi la polisi bado linawatafuta watuhumiwa wengine wawili ambao wameshirikiana na wenzao sita waliohusika namauaji yamtawa ambao ni Leonad Molleli ambapo majambazi hao wawili wana shirikiana nawenzaosita ambao ni Beda Mallya (37)Mkazi wambezi ,Michael Mushi (50)Mfanyabiashara namkazi wambezi makabe ,Sadick Kisia(32)mkazi wa mbagala kizuiani ,ELIBARIKI ELIAH makumba (40)Mkazi wabuguruni madenge Pamoja na MRUMI HAMAD SALEHE (38)mkazi wachai bora kigogo freshi’’Aliongeza Suliman Kova.
KATIKA hatua nyingine jeshi lapolisi jijini Dar es salaam limetoa angalizo kwa makapuni yaulinzi nchini wanapoajiri watumishi wao washilikiane najeshi hilo ilikuweza kufanya upekuzi unaohusika naupuimaji wa vidole na ukaguzi wa kibayolojia kufuatia majambazi kuwa natabia yakuomba kazi kwenye makapuni ya ulinzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni